Kaimu Mkurugenzi Idara ya
Usalama wa Chakula Dkt.Honest Kessy akitazama chupa ya dawa ya kuhifadhi
mahindi iliyotengenezwa na kamapuni ya Mtewele General Traders Njombe
wakati wa maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani kitaifa mkoani Njombe
leo.Kulia ni Afisa Masoko Benedicto Mgaya wa Mtewele Traders.
Kaimu Mkurugenzi Usalama wa
Chakula toka Wizara ya Kilimo Dkt.Honest Kessy (aliyevaa miwani) akipata
maelezo ya bidhaa za wajasiliamali wa wilaya ya Makete zilizoongezwa
thamani wakati alipomwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo kutembelea
mabanda ya maonesho ya siku ya chakula .Katikati ni Afisa Kilimo toka
Halmashauri ya Wilaya ya Makete Amon Mhagama akitoa maelezo kwa mgeni
rasmi .
Kaimu Mkurugenzi Mkuu Idara ya
Usalama wa Chakula Wizara ya Kilimo Dkt.Honest Kessy (aliyeva kofia
kulia) akitazama teknolojia ya kumwagilia mazao kwa njia ya asili
kutumia kisima iliyotengenezwa na kikundi cha Uvinjo Njombe.Kushoto ni
Meneja Mradi wa Uvinjo Dauson Msumange leo ikiwa ni siku ya tatu ya
maadhimisho ya Siku ya Chakula kitaifa mkoani Njombe.
Meneja wa Shirika la Taifa la
Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Njombe Mrisho Mwisimba ( kulia)
akikabidhi zawadi ya nyaraka za huduma zitolewazo na shirika hilo kwa
wakulima kwa mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo ambaye pia ni
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Usalama wa Chakula Dkt.Honest Kessy (kushoto)
alipotembelea banda hilo leo ikiwa ni siku ya Tatu ya maonesho ya Siku
ya Chakula Duniani kitaifa mkoani Njombe.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Usalama wa
Chakula ambaye pia ni mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo
Dkt.Honest Kessy (kushoto) akipokelewa na wajumbe wa kamati ya mandalizi
ya siku ya Chakula Duniani Kitaifa inayofanyik Njombe leo alipowasili
uwanja wa maonesho kwa kazi ya kukagua mabanda na kuongea na wakulima
(Picha na Wizara ya Kilimo)
……………………………………………………………………………..
Maonesho
ya Siku ya Chakula Duniani Kitaifa mkoani Njombe yamefikia siku ya
tatu mkoani Njombe ambapo mapema leo ilikuwa zamu ya Katibu Mkuu
Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya kutembelea mabanda ya maonesho na
kuzungumza na wakulima na wajasiliamali waliopo.
Hata hivyo
Katibu Mkuu amewakilishwa na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Usalama wa
Chakula Dkt.Honest Kessy ambaye amewapongeza wakulima,wafugaji na
wajasiliamali kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye maonesho ya
mwaka huu.
” Wizara
ya Kilimo inawapongeza wakulima ,wafugaji na wajasiliamali nchini kwa
kazi kubwa mnayofanya ya kuhakikisha nchi inakuwa na uhakika wa chakula
muda wote hali inayofanya uchumi wetu ukue” alisema Dkt.Kessy
Siku ya
Chakula Duniani ilifunguliwa tarehe 10 Octoba na itafikia kilele tarehe
16 Octoba ikiongozwa na kauli mbiu isemayo ” Kesho Njema Itajengwa na
Lishe Bora Endelevu”
No comments :
Post a Comment