Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba,akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani yatakayofanyika kuanzia tarehe Oktoba 10 hadi 16 Mkoani Njombe
…………………………………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Wizara ya Kilimo inapenda kuwataarifu wananchi na wadau wote wa sekta ya kilimo nchini
kuwa Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani yatafanyika kitaifa mkoani Njombe kuanzia tarehe 10 Oktoba 2020 na kilele chake itakuwa tarehe 16 Oktoba 2020.Taarifa hiyo imetolewa jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba ,amesema kuwa maandalizi ya maadhimisho hayo yamekamilika na kuwa wizara, taasisi, wakala, mashirika ya kimataifa na kitaifa zinakaribishwa kujitokeza kushiriki kwenye maadhimisho ya mwaka huu.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani mwaka huu inasema “Kesho Njema Inajengwa na Lishe Bora Endelevu”
No comments :
Post a Comment