Waziri
wa Nishati, Dkt Medard Kalemani(mwenye miwani katikati) akikata utepe
kuashiria kwa ufunguzi wa kiwanda cha kuzalisha mita za luku, cha
Multicable ltd,kilichopo katika Wilaya ya Temeke,Jijini Dar es Saalam
Waziri
wa Nishati, Dkt Medard Kalemani(mwenye miwani katikati)akifurahi mara
ya baada ya kukata utepe katika ufunguzi wa kiwanda cha kuzalisha mita
za luku cha Multicable ltd, kilichopo katika Wilaya ya Temeke, jijini
Dar es Salaam,akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wa Taasisi za Wizara
na Nishati, na wameliki wa kiwanda cha Multicable ltd
Waziri
wa Nishati, Dkt Medard Kalemani(mwenye miwani)akietembelea kwenye
maeneo mbalimbali ya kiwanda cha kuzalisha mita za luku cha Multicable
ltd, kilichopo katika Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam,akiwa
pamoja na viongozi mbalimbali wa Taasisi za Wizara na Nishati, na
wameliki wa kiwanda cha Multicable ltd
Waziri
wa Nishati, Dkt Medard Kalemani,akizungumza wakati wa ufunguzi wa
kiwanda cha kuzalisha mita za luku cha Multicable ltd, kilichopo katika
Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi
wa kiwanda cha kuzalisha mita za luku cha Multicable ltd, kilichopo
katika Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, Murtaza Alibhai
akizungumza wakati wa ufunguzi wa kiwanda hicho
Waziri
wa Nishati, Dkt Medard Kalemani(katikati) Mkurugenzi Mtendaji Tanesco
Dkt Tito Mwinuka(kulia) Mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha mita za luku
cha Multicable ltd Murtaza Alibhai , wakiwa katika ufunguzi wa kiwanda
cha kuzalisha mita za luku cha Multicable ltd, kilichopo katika Wilaya
ya Temeke, jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Nishati, Dkt Medard Kalemani(mwenye miwani katikati) akiwa katika
picha ya Pamoja na viongozi mbalimbali wa Taasisi za Wizara ya Nishati,
na viongozi mbalimbali wa kiwanda cha Multicable ltd, kilichopo katika
Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Nishati, Dkt Medard Kalemani(mwenye miwani katikati) akiwa katika
picha ya Pamoja na wafanyakazi wa wa kiwanda cha kuzalisha mita za luku,
cha Multicable ltd,kilichopo katika Wilaya ya Temeke,Jijini Dar es
Saalam
…………………………………………………………………………………………
Hafsa Omar-Dar es Salaam
Waziri
wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ametoa agizo kwa Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini( REA) pamoja na
wakandarasi wote kuhakikisha kuwa wananchi wote waliolipia huduma ya
umeme waunganishiwe umeme ndani ya siku 21.
Alitoa
agizo hilo Oktoba 5,2020 wakati akiwa kwenye ufunguzi wa kiwanda cha
kuzalisha mita luku cha Multicable Ltd kilichopo katika Wilaya ya
Temeke,jijini Dar es Salaam.
Aidha,
alisema wananchi takribani 5000 nchini wamelipia huduma hiyo na hadi
sasa hawajaunganishiwa na huduma hiyo ambayo ni muhimu katika kukuza
uchumi wa mtu mmoja mmoja na kwa nchi kiujumla.
Dkt.Kalemani,
ameleeza kuwa uwepo wa viwanda vingi vya ndani ambavyo vinazalisha
vifaa vya usambazaji wa umeme kunarahisha usambazaji wa umeme nchini na
hakuna tena sababu yoyote ambayo itapelekea ucheleweshaji wa
uunganishaji umeme kwa wananchi.
“
nimeshaeleza hapo mwanzo kuwa hakuna tena sababu zinazosababisha
wananchi wachelewe kupata umeme kwa kisingizio cha uhaba wa mita za
luku, kwenye kiwanda hiki ambacho nimekifungua leo kuna takribani mita
za luku 500,000 ambazo zipo tu hata hazijanunuliwa”alisema
Dkt.Kalemani.
Pia,
amewataka wakandarasi wanaotekeleza mradi wa REA kukamilisha kazi zao
ifikapo tarehe 15 Oktoba mwaka huu, kwakuwa vifaa vyote vinavyohitaji
kwaajili ya usambazaji umeme vinapatikana kwenye viwanda nchini,ambavyo
ni vya bei rahisi na vyenye ubora wa viwango vya juu.
“wakandarasi
wote ambao miradi yao imekaribia kukamilika ambao wengi wao amebakiza
vijiji 2 au 3, wakamilishe kazi zao kwa haraka na hatutawaongezea muda
na ifikapo Oktoba 15 mwaka huu wakabidhi miradi yao”alisema.
Aidha,
amewataka wananchi wote ambao hawajafikiwa na huduma ya umeme kwenye
maeneo yao nchini watulie, na kuamini Serikali yao, kwani tayari
Serikali imeshatekeleza miradi mingi na mpango wa Serikali ni
kuhakikisha kuwa umeme unafika kwa wananchi wote ambao hawajafikishiwa
umeme ndani ya miaka miwili ijayo.
Alieleza
kuwa, Serikali imejipanga vizuri kuhakikisha huduma ya umeme
inapatikana nchini kote na kuwataka wawekezaji nchini kuendelea kufungua
viwanda vingi zaidi vya vifaa vya usambazaji wa umeme,ambapo ameeleza
kuwa kufunguliwa kwa viwanda vingi kutawarahisishia wananchi kupata
umeme kwa muda mfupi zaidi.
Amesema,
Serikali itahakikisha inavilinda viwanda vyote vya kuzalisha mita za
luku nchini ambavyo mpaka sasa vimefunguliwa viwanda takribani 10 vya
uzalishaji huo, ambavyo vinasaidia kutaoa ajira nyingi kwa watanzania na
Serikali imejipanga kuhakikisha inavilinda viwanda hivyo kwa
kuwatafutia soko la kuzia bidhaa zao.
Pia,
amewashukuru wawekezaji wa viwanda vya kutengenezea vifaa vya
kusambazaji umeme nchini,viwanda hivyo ambavyo vimesaidia sana kutatua
changamoto ya upatikanaji wa vitendea kazi vya usambazaji umeme nchini.
Vilevile,
amewahamasisha wawekezaji mbalimbali nchini kuendelea kuwekeza katika
viwanda vya kuzalisha mita za kusambazia gesi majumbani.
Ambapo
ameeleza kuwa, tayari Serikali imeshaweka zuio kwamba ifikapo januari
wakandarasi wote watakaopewa kazi ya usambazaji gesi majumbani
hawataruhusiwa kuagiza mita kutoka nje ya nchi ili kulinda soko la
ndani.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa kiwanda cha Multicable ltd , Murtaza Alibhai
amesema kuwa wameamua kutekeleza sera ya Rais wa awamu ya tano, ya
Tanzania ya viwanda kwa vitendo ili kuendana na kasi ya ukuaji wa uchumi
nchini, ambapo amesema kiwanda hicho mpaka sasa kimeajiri zaidi ya
wafanyakazi 700.
Amesema
kiwanda chao kitahakikisha kuwa kinazalisha bidhaa bora zenye viwango
vya hali ya juu ili kuchangia uchumi kupitia sekta ya viwanda.
Aidha,
ameeleza kuwa kampuni hayo inatarajia kuanzisha kiwanda cha kutengeneza
transifoma hivi karibuni ili kuhakikisha kuwa usambazaji umeme nchini
unafanyika kwa haraka na watanzani wote wafurahiye kupata huduma ya
umeme.
No comments :
Post a Comment