Meneja
wa Mradi wa ENRICH, Bi Mwivano Malimbwi (aliyesimama) akitoa mafunzo
maalum ya malengo ya mradi huo ya utoaji wa elimu ya lishe na kuboresha
afya ya uzazi kwa vijana balehe kwenye mikoa ya Singida na Shinyanga
kwa waandishi wa habari ya Mkoa wa Singida (hawapo pichani) leo, aliyekaa ni mtaalam wa Jinsia na Utetezi wa Mradi huo Tumaini Fred
Mkuu
wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi akiangalia mazao ya asali na
mashine ya kukamulia asali ya kikundi cha ufugaji wa nyuki mkoani
Singida kinachofadhiliwa wa World Vision
**
Na. John Mapepele,Singida
Shirika
la World Vision nchini limewataka waandishi wa habari kama wadau wakuu
wa Shirika hilo kutoa taarifa sahihi za kazi za shirika hilo kwenye
mradi wake wa ENRICH ambao unatekelezwa katika mikoa ya Singida na
Shinyanga.
Mradi
huo unalengo la kupeleka elimu ya lishe na afya ya uzazi kwa vijana
balehe vijijini ili kupunguza vifo vya akinamama wajawazito na watoto
chini ya siku 1000 na ili kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu
ya Tano ili kuboresha maisha ya watanzania.
Akitoa
mafunzo maalum kuhusu malengo wa mradi kwa waandishi wa Mkoa wa
Singida , Meneja wa Mradi wa ENRICH Bi, Mwivano Malimbwi amesema mradi
huu ni wa miaka mitano kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka 2021 na
umejikita katika kuwezesha huduma za lishe ili kuimarisha afya ya
mama na mtoto kwa gharama za dola milioni 8.4 za Canada.
Kwa
mujibu wa Malimbwi malengo mahususi ya ENRICH ni kupunguza vifo vya
akina mama na watoto kwa kuangalia visababishi vya vifo hivyo ambapo
mradi umeelekeza nguvu kwenye kuimarisha mifumo ya utoaji wa afya katika
vituo vya kutolea huduma hizo.
Aliongeza
kuwa awali wakati mradi ulipoanza walibaini changamoto ya upatikanaji
wa vifaa vya kumchunguza hali ya kiliishe ya mtoto vilikuwa na
upungufu mkubwa ambapo vituo vichache vilikuwa na vifaa hivyo vya
kupimia urefu na mzingo wa kati wa mkono kwa akina mama na mtoto.
Alisema
watoa huduma wachache walipata mafunzo ya afya ya lishe kwenye ngazi
ya mkoa na wilaya ambapo hakukuwa na watoa huduma katika maeneo ya
vijijini.
Aidha
alisema pia hakukuwa na elimu ya uongozi kwenye kamati za afya za
mikoa na wilaya ambapo Mradi uliwajengea uwezo ili kuwa sehemu ya
kuleta mabadiliko kwa pamoja badala ya kuwa watoa maamuzi.
Aidha mipango na bajeti ilikuwa ikifanywa kwa hisia badala ya kutumia takwimu sahihi.
Malimbi
amesema lengo la pili la Mradi ni kuongeza uzalishaji wa chakula
chenye uwingi wa virutubisho ambapa kwenye eneo hili amessisitiza kuwa
mkakati umekuwa katika kuongeza uzalishaji ulioongezwa kibailojia,
kuongeza utumiaji wa virutubishi kwa watoto na sayansi ya ulaji na
ufyonzaji wa virutubishi.
Alisema
pia katika mikoa ya Singida na Shinyanga imebarikiwa kuwa na vyakula
vya makundi yote na matunda ya asili kama sasati, rade na furu ambayo
kama yakitumika kikamilifu yatasaidia sana kuboresha lishe na kupunguza
udumavu kwa watoto.
Alipongeza
jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Dk. Rehema Nchimbi kuwa
mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa suala la lishe na afya ya uzazi
vinakuwa kipaombele cha kwanza kwa wananchi ambapo pia amesema
amehamasisha ulaji na ulimaji wa viazi lishe na kuwafanya wananchi wa
Mkoa wa Singida tofauti na awali ambapo vilikuwa vikiuzwa nje ya Mkoa.
Aidha
amesema Mradi umehamasisha akina mama kulima bustani za mbogamboga
kwenye kila kaya ili kuhakikisha kuwa kwenye kila mlo mboga zinakuwepo.
Amesema
lengo la mwisho la mradi huo ni kuhakikisha kuwa kunakuwa na
uwajibikaji wa wadau wote muhimu na kila mmoja anafanya majukumu yake
kwa ufasaha, ambapo ametolea mfano kuwa Serikali kama mdau mkuu ina
wajibu wa kuweka vituo vya kutolea huduma na mtoa huduma ambapo jamii
inawajibu wa kuvitumia vituo hivyo na watoa huduma.
Mradi
wa ENRICH ni Mradi wenye sekta nyingi na unafadhiliwa na Serikali ya
nchi ya Canada ambapo unatekelezwa kwa kushirikiana na wabia ambao ni
Nutritional International, Canadian Society for International Health
anayejikita katika kuimarisha mfumo wa afya.
Ikiwemo
Harvest Plus, kwenye Sekta ya Kilimo, Chuo kikuu cha Toronto katika
kufanya tathimini na ufuatiliaji wa mradi na World Vision ambaye ni
msimamizi mkuu wa fedha wa mradi huo. Serikali ya Tanzania ni
mtekelezaji namba moja chini ya TAMISEMI.
No comments :
Post a Comment