Na.Faustine Galafoni,Dodoma.
Katika
kukabiliana na changamoto ya uhaba wa vitabu vya kujifunzia katika vyuo
vya kilimo hapa nchini,Wizara ya kilimo imeamua kugawa vifaa vya
kielektroniki katika vyuo 14 vya kilimo nchini vyenye thamani ya
Tsh.Milioni 248.69.
Akizungumza
na waandishi wa Habari Agosti,31,2020 jijini Dodoma katika hafla fupi
ya ugawaji wa vifaa hivyo vya TEHAMA , Katibu mkuu Wizara ya Kilimo
Gerald Msabila Kusaya amebainisha kuwa tangu ateuliwe kuwa katibu Mkuu
wa Wizara hiyo tarehe 5,Machi mwaka huu amebahatika kufanya ziara
katika vyuo mbalimbali vya elimu ya kilimo hapa nchini na kubaini
changamoto ya uhaba wa vitabu hivyo na kuamua kununua vifaa vya
kielekroniki kwa ajili ya kujifunzia .
“Baada
ya kuona changamoto hiyo tulijadili na wadau tukaona namna nzuri ya
kusoma kwa njia ya kielekrtoniki hivyo tumeamua kununua kununua vifaa
mbalimbali hali itakayosaidia wanafunzi wetu ambao ni wataalam wa baadae
wa kilimo kujifunza kwa njia ya mtandao na vifaa hivyo vikigharimu
Tsh.Milioni 248.69 “amesema.
Aidha,Katibu
mkuu huyo wa Wizara ya kilimo ametoa wito kwa wakuu wa vyuo vya kilimo
kuhakikisha wanasimamia vinatumika vizuri na mara kwa mara ili kuwandaa
wataam wa kilimo wanaoendana na wakati.
Wakitoa
neno la shukrani baada ya kupokea vifaa hivyo kwa niaba ya Wakuu wa
vyuo 14 vya serikali,mkuu wa chuo cha Kilimo Mlingani Samson Cheyo
pamoja na kaimu mkuu wa chuo cha Sukari [National Sugar Institute-NSI]
Kilichopo Kilombero Mkoani Morogoro Aloyce Kasmir wamesema vifaa hivyo
vya TEHAMA vitarahisisha katika ufanisi wa kujifunza.
Baadhi
ya vifaa vya TEHAMA vilivyotolewa ni pamoja na Rooter Machine,Kompyuta
mpakato[laptop],Desk top,TV vikiwa na thamani ya Tsh.Milioni 248.69.
No comments :
Post a Comment