Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ( kulia)
akizungumza na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Donald Wright
kuelezea mafanikio ya Tanzania katika Uhifadhi wa Maliasili na utayari
wa Tanzania kupokea Watalii kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Marekani
wakati huu wa janga la Corona. Mazungumzo hayo yamefanyika jijini Dar es
Salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.
Hamisi Kigwangalla ( kulia) akimwomba Balozi wa Marekani nchini
Tanzania Dkt. Donald Wright (kushoto) asaidie kuwahamasisha raia wa
Marekani na watu maarufu wakiwemo Wasanii wakubwa wa Marekani na vilabu
mbalmbali maarufu vya michezo vitembelea vivutio vya utalii vya
Tanzania alipokutana nae kwa mazungumzo mafupi jijini Dar es salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ( kulia) na
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Donald Wright (kushoto) Wakiwa
katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo mafupi
yaliyolenga kukuza Utalii hasa wakati huu wa janga la Corona na
kuendeleza ushirikiano baina ya Tanzania na Marekani katika shughuli za
uhifadhi.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ( katikati)
akitoa ufafanuzi kwa Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Donald
Wright (kushoto) na ujumbe wake kuhusu namna Tanzania ilivyofanikiwa
kulinda maeneo yaliyohifadhiwa, kudhibiti ujangili pamoja na Taifa
kuendelea kunufaika kimapato, kutoa fursa za ajira na uwekezaji kwa
Watanzania na Wageni akimwomba Balozi huyo asaidie kuhamasisha raia wa
Marekani waje kuwekeza nchini Tanzania.
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Donald Wright (kushoto)
akimweleza jambo Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla
(kulia) walipokutana kwa mazungumzo mafupi yaliyojikita katika
kuimarisha ushirikiano na uendelezaji wa shughuli za uhifadhi baina ya
Tanzania na Marekani leo jijini Dar es salaam
Balozi
wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Donald Wright (kulia) akitoa
ufafanuzi kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla
kuhusu mchango wa Taifa la Marekani katika shughuli za Uhifadhi nchini
Tanzania na namna nchi yake itakavyoendelea kusaidia shughuli za
uhifadhi katika eneo la Mafunzo, Teknolojia na Vitendea kazi
walipokutana kwa mazungumzo jijini Dar es salaam.
PICHA/Aron Msigwa – WMU.
No comments :
Post a Comment