Saturday, September 5, 2020

WAZIRI SIMBACHAWENE AIHAKIKISHIA MAREKANI KUWA NCHI IPO SALAMA KWA RAIA NA WAGENI


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto), akimsikiliza Balozi wa Marekani Nchini, Dkt. Donald Wright alipokuwa akizungumza masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani, jijini Dodoma, leo. Simbachawene amemhakikishia balozi huyo kuwa, Tanzania ipo salama na itaendelea kuwa salama kwa raia wake na wageni mbalimbali waliopo na wanaoingia nchini. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto) akizungumza na Balozi wa Marekani Nchini, Dkt. Donald Wright, wakati alipomtembnelea ofisini, Mji wa Serikali, Mtumba, jijini Dodoma, leo. Simbachawene amemhakikishia Balozi huyo kuwa, Tanzania ipo salama na itaendelea kuwa salama kwa raia wake na wageni mbalimbali waliopo na wanaoingia nchini. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto) akimuaga Balozi wa Marekani Nchini, Dkt. Donald Wright, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika, Mji wa Serikali, Mtumba, jijini Dodoma, leo. Simbachawene amemhakikishia Balozi huyo kuwa, Tanzania ipo salama na itaendelea kuwa salama kwa raia wake na wageni mbalimbali waliopo na wanaoingia nchini. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (wapili kushoto), Balozi wa Marekani Nchini, Dkt. Donald Wright (katikati), wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika, jijini Dodoma. Simbachawene amemhakikishia Balozi huyo kuwa, Tanzania ipo salama na itaendelea kuwa salama kwa raia wake na wageni mbalimbali waliopo na wanaoingia nchini. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
******************************
Na Mwandishi Wetu MOHA-Dodoma
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene ameihakikishia Marekani kuwa, Tanzania ipo salama na itaendelea kuwa salama kwa raia wake na wageni mbalimbali waliopo na wanaoingia nchini.
Akizungumza na Balozi mpya wa Marekani Nchini, Dkt Donald Wright, ofisini kwa Waziri huyo, Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma, leo, Simbachawene amesema usalama wa nchi upo juu na kwamba tumefanya vizuri katika kutambulisha wageni katika maeneo ya uwekezaji na utalii.
“Mheshimiwa Balozi nikuhakikishie tu, nchi yetu ipo salama sasa kuliko wakati mwingine wowote, na hatujawahi kuwa na kesi za ajabu, hii kutokana na uimara wa Serikali ya Rais Magufuli ambayo ipo wazi na imefanikiwa kudhibiti rushwa,” alisema Simbachawene.
Pia Waziri Simbachawene alisema Serikali inaendelea kudhibiti biashara haramu ya binadamu ambapo mpaka sasa imeweza kuwarudisha Wasomali 1,300,000 wanaopita nchini kwenda Afrika Kusini.
“Mafanikio haya ya kudhibiti biashara hii haramu ya binadamu ni kutokana na kuwepo kwa sheria ya mwaka 2008 na kanuni zake ambapo imeweza kutusaidia kudhibiti biashara hii kwa kutumia sheria za nchi,” alisema Simbachawene.
Aliongeza kuwa, mipaka ya nchi ipo imara na Serikali inaendelea kuimarisha zaidi ambapo imeweza kudhibiti watu wanaoingia na kutoka katika mipaka mbalimbali nchini.
Kwa upande wake Balozi Dkt. Wright aliipongeza Tanzania inavyoshughulikia biashara haramu ya binadamu na alikiri hajawahi kukutana na kesi za ajabu zinazohusiana na biashara hiyo.
“Watanzania watu wakarimu, wastaarabu na wenye furaha wakati wote, hivyo nafurahi kuwa Tanzania kama Balozi wa Nchi hii, na Marekani itaendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali” alisema Balozi Dkt. Wright.
Pia Waziri Simbachawene alimuhakikishia Balozi huyo kuwa, Serikali itaendelea kushirikiana na Marekani katika maeneo ambayo yana maslahi kwa Tanzania na Marekani.

No comments :

Post a Comment