Mstaafu mtarajiwa akiwa na mwenzi wake
wakitafakari juu ya maandalizi ya kustaafu.(Na Mpigapicha
Wetu)
Na Christian Gaya, Majira Ijumaa 04 Septemba 2020
Kustaafu
huhitaji wa muda wa kupumnzika, kuburudika na kula matunda na ya nguvukazi yako
ulipokuwa mtumishi kwa miaka yote. Ni wakati mdau kukaa na kutulia kwenye...
nyumba yake aliyokuwa amejenga kijijini kwake au mjini, kutembelea mbuga za
wanyama au sehemu nyingine yoyote ile, ni wakati wa kucheza na wajukuu wake.
Baada
ya hapo unatakiwa kurudi kwenye ndoto yako ya kipaji chako ulichopewa na
Mwenyezi Mungu ulichotaka mara kwa mara kukifanyia kazi, ambapo ulipoajiriwa
ulikuwa unashindwa kwa sababu huenda muda mwingi ulikuwa unamtumikia mwajiri
wako.
Kwa
aina ya maisha yeyote utakayochagua kuishi baada ya kustaafu, kitu muhimu
ambacho ni kukumbuka sana kutodhubutu kufanya yaani mtindo wa mkono kinywani
bila kujishughulisha na kazi yeyote ya kukuongezea kipato.
Unatakiwa
kujiwekee muda wa kustaafu mapema, ikiwezekana kabla ya kufika tayari muda wa
kuachia ngazi ya kazi yako kwa mwajiri wako akilini, kwa maana ya mwaka na hasa
wakati wowote ambapo bado una nguvu zako za kutosha za kuweza kujiandaa mapema
kwa ajili ya kustaafu na si kusubiri mpaka mwaka wa kustaafu kwako utakapofika
au kukaribia hodi.
Hivyo
wakati huo sekta rasmi au sekta isiyo kuwa rasmi itakuwa ndiyo njia ya maamuzi
yako kuingia huko kuendelea na shughuli zako baada ya kustaafu kama bado hali
ya afya yako itakuruhusu kufanya hivyo, lakini pamoja na kutegemea kujiunga na
sekta isiyo rasmi itategemea na fursa ulizonazo, pamoja na baadhi ya raslimali ikiwemo
na akiba yako ya fedha ulizonazo.
Kumbuka
ya kuwa mapato ya mtu mara nyingi hupungua hasa pale baada ya kustaafu labda
mtu awe na biashara ambayo haimshirikishi yeye na biashara yenyewe iwe labda na
mapato makubwa. Kwa sababu hata njia nyingi za vyanzo vya mapato wakati
mwingine hupungua kama vile mikopo mbalimbali ambayo hutumia mshahara wako kuwa
ndiyo dhamana ya kupatiwa mikopo hiyo. Ingawa kuna baadhi ya mabenki hutumia
pensheni za wastaafu za kila mwezi kama dhamana ya kuwakopesha baadhi ya
wastaafu.
Kwa
bahati mbaya sana, huwezi ukaamini ya kuwa utafiti unaonesha ya kuwa karibu
asilimia themanini (80%) ya nguvukazi ya Afrika Mashariki siyo wanachama wa
mifuko ya hifadhi ya jamii. Kwa hapa Tanzania ni asilimia 6 tu ya nguvukazi
ndiyo wanalio katika mifuko ya hifadhi ya jamii, wakati kwa Kenya ni asilimia
20 ya nguvukazi na Uganda ambapo ni sawa na asilimia 16 tu ya nguvukazi ndiyo
wanaohudumiwa na mifuko ya jamii tu.
Kwa
hiyo ina maana ya kwamba itakapofikia mwaka wa kustaafu kundi hili halitaweza
kujitegemea lenyewe pamoja ya kuwa karibu miaka yote wamekuwa wakifanya kazi.
Na kama hutaki kuingia katika kundi hili, hebu jaribu kufahamu mambo muhimu
yanayoweza kukusaidia kujiandaa kustaafu bila hofu yeyote ile.
Kama uko kwenye umri wa miaka 20
au mapema ukiwa na umri wa miaka 30 kustaafu kwako kunaonekana ni mbali sana
kuanzia umri huo, lakini kumbe ndiyo muda mzuri wa kuanza kuweka akiba yako kwa
ajili ya kustaafu baadaye. Pamoja na hayo yote ni kwamba kwa sasa una majukumu
machache ukilinganisha na mtu ambaye yupo kazini muda mrefu na anakaribia
huenda kustaafu.
Kwa sasa unatakiwa kujiunga na Mfuko
Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kama umeajiriwa kwenye sekta rasmi au
umejiajiri mwenyewe kwenye sekta isiyorasmi, na kama ni mtumishi wa umma basi
jiunge na Mfuko wa hifadhi ya jamii kwa ajili ya watumishi wa umma (PSSSF)
pamoja na kujiunga na Mfuko wa hifadhi ya jamii wa Zanzibar ZSSF
Jiunge haraka iwezekanavyo ili
uweze kunufaika na mafao ya muda mrefu kama vile pensheni ya kustaafu, pensheni
ya ulemavu, pensheni ya urithi, na mafao ya muda mfupi ni kama vile mafao ya
uzazi, mafao ya kuumia kazini, mafao ya matibabu na mafao ya msaada wa mazishi.
Mifuko pia hutoa amana ya mikopo ya nyumba ya makazi wakati huo huo
unapoelendelea na kazi. Hivyo usipoteza miaka yako ya faida na mapato
yanayovutia yapotee bure bila kuweka akiba na kuwekeza.
Kampuni nyingi za bima hazitoi
bima za afya kwa ajili ya watu waliofikia umri mkubwa zaidi kulingana na
taratibu na miongozo ya bima. Na hata wakitoa hiyo bima ya afya kwa mzee zaidi
inaweza kuwa na tozo kubwa mno. Kumbuka kwa sasa tuna mifuko ya hifadhi ya
jamii inayotoa mafao ya matibabu kama vile NSSF na Mfuko wa taifa wa bima ya
afya (NIHF)
Baada ya kustaafu katika kampuni
iliyokuwa ukipata bima ya afya na familia yako kwa kukulipia kila mwezi gharama
za matibabu, sasa unatakiwa ujiunge na mifuko ya hifadhi ya jamii ili usije
ukapata hofu na kuanza kulipa mwenyewe gharama za matibabu kutoka mfukoni mwako
na hatimaye kukusababishia mshituko wa moyo.
Tambua ya kuwa kampuni nyingi
zinasimamisha huduma ya bima ya afya mara tu baada ya wewe kuacha kazi au kustaafu.
Kwa hali hii kunaweza
kukusababishia kuanza kuwa na matumizi makubwa ya fedha, na hivyo kukupelekea
kuanza kula akiba yako yote na kukuacha na bila kitu chochote katika maisha
yako yote na familia yako. Na ndiyo maana kuna umuhimu mkubwa wa kuanza kujiunga
na mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo inatoa mpango mahususi wa bima ya afya yaani
fao la matibabu haraka iwezekanavyo.
Wakati upo kwenye mpito wa kutoka
kampuni moja na kujiunga na nyingine pengine, unatakiwa kuwa mwangalifu na makini sana, kwa
sababu unaweza kushawishika kutaka kuondoa michango yako ya pensheni. Hapa
ukiwa na mategemeo makubwa ya kuwa unakokwenda huko kwa mwajiri mpya utakuwa
unapata mshahara mnono na marupurupu mengi. Kinachotakiwa hapa ni kwenda
kumwonesha mwajiri wako mpya kadi yako ya uanachama ili aendelee kukuchangia kwenye
akaunti yako hiyo hiyo ya zamani ili kutunisha pensheni yako ya baadaye.
Labda uwe umejipanga vizuri sana
vinginevyo hiyo michango ya pensheni uliyochukua itaishia kutumika tu bila hata
kuwekezwa kwenye vitega uchumi. Na utafiti unaonesha ya kuwa wafanyakazi wengi
wanaochukua michango yao kabla ya kuiva kufikia kuwa pensheni hawawekezi katika
vitega uchumi kama vile kwenye hatifungani za muda mrefu na za muda mfupi.
Wakati mwingine unapochukua
michango ya pensheni kabla ya wakati wake inaishia kukatwa faini kwa kuchukua
kabla ya muda wake haujafika na kuanza kulalamika kwamba ni kidogo bila ya
kujua ya kuwa huenda hata mahesabu yake hayakufanywa kwa utaratibu na kanuni
zinazotakiwa kisheria.
Mwandishi
wa Makala hii ni mwanzilishi wa Kituo cha HakiPensheni, mshauri na mtaalamu wa
masuala ya pensheni. Kwa maelezo zaidi: gayagmc@yahoo.com unaweza kutembelea hakipensheni
website, Simu +255 655 13 13 41,
info@hakipensheni.co.tz
No comments :
Post a Comment