- Mkuu wa Kitengo cha Elimu, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Faraja Chiwanga akifunga mafunzo ya mbinu za utafiti yaliyofanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila.
Method Kazaura kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi
Muhimbili- MUHAS- akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wawezeshaji wa
mafunzo hayo.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi Muhimbili-Mloganzila Sis.
Redemptha Matindi akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mafunzo ya mbinu
za utafiti mara baada ya kuhitimishwa mapema hii leo.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Julieth Magandi akiwakabidhi vyeti wahimu wa mafunzo ya mbinu za utafiti.Dkt. Julieth Magandi akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo hayo.
*************************************************
Watumishi katika sekta ya afya wasisitizwa umuhimu wa kufanya
tafiti katika maeneo yao ya kazi ili kuendelea kuboresha utoaji wa
huduma za afya nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa
Kitengo cha Elimu, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu kutoka
Hospitali ya
Taifa Muhimbili Dkt. Faraja Chiwanga wakati akihitimisha mafunzo ya siku
tano ya mbinu za utafiti yaliyofanyika katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili-Mloganzila.
Akizungumza kwa niaba ya
Mkurugenzi Mtendaji Prof. Lawrence Museru, Dkt. Chiwanga amesema
wataalamu wa sekta ya afya hawanabudi kujikita katika kufanya tatifi ili
kuboresha njia mbalimbali za kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa.
“Tukijike katika kufanya tatifi
ili kuleta mapinduzi katika sekta ya afya, hivyo tutumie mafunzo haya
kwa vitendo kwa kuandika tafiti mbalimbali kwa maslahi ya taifa letu”
amesema Dkt. Chiwanga.
Jumla ya washiriki 25 wa kada mbalimbali wamehitimu hayo
yaliyotolewa na wataalamu wabobezi katika tafiti za afya kutoka Chuo
Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili- MUHAS- kwa kuratibiwa na
Kitengo cha Elimu, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu MNH-Mloganzila.
No comments :
Post a Comment