WAKUU
WA Idara na vitengo wakiwa katika picha moja mara baada ya kumaliza
kutoa maoni juu ya uratibu wa miongozo ya kimataifa yaliyotolewa na
Wataalam toka Wizara ya Kilimo na Mifugo kwa kushirikana na Shirika la
kilimo na chakula Duniani FAO juu ya Uboresaji wa Sekta ya Uvuvi mdogo
Nchini.Picha na Ofisi ya Ded Nyasa.
**********************************
Na Netho Credo,Nyasa
Hapo jana katika Ofisi ya
Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa, kumefanyika Mkutano wa
timu tendaji
kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na wakuu wa idara na Vitengo, Mkutano
wenye lengo, la kuchukua maoni ili kuendeleza Sekta ya Uvuvi Mdogo
nchini kwa Muktadha wa kuhakikisha Usalama wa Chakula na kupunguza
umaskini.
Mkutano huo umeendeshwa na watalam
kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na uratibu wa Shirika
la Kilimo na chakula Duniani FAO ambao imeandaa mwongozo wa hiari,
unaoelekeza misingi na masuala ya muhimu ya kuzingatia ili kurahisisha
ushughulikiaji wa maendeleo ya sekta ya uvuvi mdogo katika nchi yoyote
ulimwenguni.
Aidha washiriki walipata fursa ya
kubainisha changamoto zinazowakabili wavuvi na kutoa suluhisho nini
kifanyike ili wavuvi waboreshewe maslahi.vitendea kazi vya kisasa na
kuwa na jamii yenye maendeleo.
Lengo kuu la kutekeleza mwongozo
wa kimataifa unaohusu uvuvi mdogo ni kuhakikisha nchi yetu inatunza
raslimali za uvuvi, kwa ajili ya kizazi cha sasa na kuhakikisha
uzalishaji wa mazao ya uvuvi yanaongezeka, na hivyo kuchangia katika
kuhakikisha usalama wa chakula nchini na kuboresha hali ya uvuvi ikiwa
ni pamoja na kupunguza umaskini miongoni mwa wanajamii yauvuvi.
Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi
Bw.Bernad Semwaiko alizitaja Baadhi ya changamoto zinazoikabili Sekta ya
Uvuvi Wilayani hapa ni Ukosefu wa Zana za kisasa za uvuvi, kwa kuwa
wavuvi wengi hutumia zana duni kwa ajili ya Uvuvi, Ukosefu wa elimu ya
Uvuvi, kwa kuwa kwa sasa wavuvi wengi wanavua kama Utamaduni wa Kabila
la Wanyasa.
Serikali kupitia Wizara ya mifugo
na uvuvi inaratibu zoezi la kuandaa mpango kazi utakaotumika katika
kutekeleza mwongozo huo wa kimataifa wa Uvuvi mdogo.
No comments :
Post a Comment