Mkurugenzi
wa elimu kwa mlipa kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Richard Kayombo
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)leo jijini Dar es
Salaam leo.
Na Ripota wetu, Michuzi TV
MAMLAKA
ya mapato Tanzania (TRA) imewataka waajiriwa wote ambao wanalipwa
mshahara kwa payroll kuwa na TIN namba na kuziwasilisha kwa waajiri
wao.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, Mkurugenzi wa elimu
kwa mlipa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA,) Richard Kayombo
amesema kuwa kuanzia mchakato hua umeanza mwezi Agosti, 2020 na mwisho
wa kuwasilisha TIN hizo ni Desemba 31, 2020.
"Mtumishi ambaye ameajiriwa popote pale anatakiwa kupata TIN namba na kuiwasilisha kwa mwajiri wake." Amesema Kayombo.
Hata
hivyo amesema kuwa mwajiriwa ambaye amepoteza TIN namba au hana afike
ofisi za TRA ili aweze kupata TIN nyingine na kwa ambaye hana kabisa
atembelee tovuti ya TRA ili aweze kuipata.
"Zoezi
hili ni la watumishi walioajiriwa popote pale wawasilishe TIN kwa
mwajiri litadumu hadi Desemba 31,2020, kwahiyo waajiri wote
tumeshawaagiza wahakikishe wafanyakazi wao wamewasilisha TIN zao."
Na kwa mwajiriwa ambaye hakuweza kupeleka TIN Kwa mwaajiri wake hataweza kupata mshahara ifikapo Januari mosi, 2021.
Kayombo
amesema kuwa hakuna haja ya kuongeza muda kwa kuwasilisha TIN au kodi
za mshahara kwa sababu TIN hizo zinawasikishwa kwa njia ya mtandao
popote mtu alipo anaweza kuwasilisha.
"Kwa
kipindi hiki tumerahisisha kwa kila mtu kutumia mtandao ili kuondoa
usumbufu kwa mtu yeyote kufika ofisi za TRA." Amesema Kayombo.
Hata hivyo Kayombo amesema kuwa kampeni ya Mlango kwa Mlango imeendelea kuwafikia watu wengi zaidi.
Amesema
kampeni ya Mlango kwa mlango kwa Septemba watafanyia kazi katika mikoa
michache ambayo ni Arusha, Mtwara, Kagera Tabora na Mkoa wa Dar es
Salaam watafanyia kazi katika wilaya ya Ubungo.
Amesema
Kampeni ya Mlango kwa Mlango ni mahususi kuwafikia walipa kodi katika
biashara zao na kutomsumbua mfanyabiashara kufika katika Ofisi za TRA.
No comments :
Post a Comment