Thursday, September 10, 2020

Nchi za Ulaya Zahimizwa Kuondoa Vizuizi vya Kusafiri


Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Mhe. Jestas Nyamanga akiongoza Mkutano maalum wa mashauriano kati ya Jumuiya ya nchi za Afrika, Carribean na Pacific (OACPS) na ujumbe waUjerumani uliokuwa ukingozwa na Waziri wa Masuala ya Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo wa Serikali ya Shirikisho la Ujerumani, Dkt. Gerd MÙLLER ambayo kwa sasa nchi hiyo ni Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Mhe. Jestas Nyamanga akiongoza Mkutano maalum wa mashauriano kati ya Jumuiya ya nchi za Afrika, Carribean na Pacific (OACPS) na ujumbe wa Ujerumani uliokuwa ukingozwa na Waziri wa Masuala ya Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo wa
Serikali ya Shirikisho la Ujerumani, Dkt. Gerd MÙLLER ambayo kwa sasa nchi hiyo ni Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya.
Mhe.BaloziNyamanga kwa nafasi yake ya Mwenyeki wa Mabalozi wa OACPS akimtambulisha Waziriwa Ushirikiano wa Ujerumani Mhe. Dkt. Muller na timu yake katika Ukumbi wa OACPS.

Mhe. Balozi Nyamanga akimsindikiza Mgeni wake Mhe.Dkt.Muller nje ya ukumbi wa mkutano baada ya mkutano wa mashauriano kukamilika.

Jumuiya ya nchi za Afrika, Carribean na Pacific (OACPS) imetoa wito kwa Umoja wa Ulaya kuondoa vizuizi vya kusafiri (travelbans) kwa baadhi ya nchi za OACPS hususan zile zilizoonesha kuwa salama zaidi dhidi ya maambukizi ya Ugonjwa wa Corona kama Tanzania. 
 
Wito huo ulitolewa katika kikao maalum cha mashauriano baina ya Jumuiya ya nchi za OACPS na nchi ya Ujerumani ambayo kwa sasa ni Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya.

Mashauriano hayo yaliyofanyika tarehe 9 Septemba2020 katika Ofisi za Jumuiya ya OACPS, Brussels nchini Ubelgiji, yaliongozwa naBalozi wa Tanzania nchini Ubelgiji na Mwakilishi wa Tanzania katika Umoja waUlaya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mabalozi wa nchi za OACPS walioko Brussels,Mhe. Jestas Abuok Nyamanga na ujumbe wa Ujerumani uliongozwa na Waziri wa Masuala ya Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo wa Serikali ya Shirikisho laUjerumani, Dkt. Gerd MÙLLER.

Katika kikao hicho wajumbe walisisitiza umuhimu wa Umoja wa Ulaya kuendelea kuunga mkono Shirika la Afya Duniani (WHO) katikakusimamia ithibati za tafiti za chanjo za ugonjwa wa Corona na Shirika hilokuendelea kujengewa uwezo wa kusimamia utaratibu wa kuhakikisha kuwa chanjo
itakayothibitika inawafikia mataifa yote kwa usawa na kwa gharama nafuu.

Kikao hicho kilijadili pia hatua mbalimbalizinazopaswa kuongeza msukumo kwa Umoja wa Ulaya katika kuzisaidia nchi za OACPSkukabiliana na athari za kiuchumi zinazotokana na ugonjwa wa Corona hususankatika sekta ya utalii na kilimo. Mikakati iliyojadiliwa ni pamoja na ileinayolenga kupunguza, kufuta au kubadilisha masharti ya ulipaji wa madeni yanchi za Jumuiya ya OACPS na wito wa nchi za OACPS kuutaka Umoja wa Ulayakusogeza mbele utekelezaji wa baadhi ya kanuni na taratibu mpya za biasharazilizopangwa kuanza kutumika mwanzoni mwa mwaka ujao ili kuzipa nafasi nchi zaOACPS kujipanga zaidi kabla ya kuanza kutumia kanuni hizo.

Kupitia mashauriano hayo, pande zote mbilizilitathmini mwenendo wa majadiliano ya Mkataba mpya wa ubia wa Ushirikiano waKiuchumi baina ya nchi za Jumuiya ya OACPS na Umoja wa Ulaya yanayoendelea hivisasa baada ya mkataba wa sasa kufikia kikomo mwezi Desemba 2020. Pande mbilizilijadili kwa kina namna ya kushirikiana katika maeneo yanayolenga kuongeza mnyororo wa thamani ya mazao ya kilimo, uwiano ulio sawa katika biashara na maendeleo ya teknolojia katika kukuza uchumi na maendeleo ya watu.

Kikao kilihitimishwa kwa Ujerumani kuonesha utayariwa kuyapa kipaumbele masuala yote yaliyojadiliwa katika kipindi cha uongoziwake wa Baraza la Umoja wa Ulaya na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano waAfrika Mashariki katika kipindi hiki ambacho inashika nafasi ya Rais wa Barazala Mawaziri wa nchi 79 wanachama wa Jumuiya ya nchi za Afrika, Carribean na Pacific itaendelea kushirikiana na Umoja wa Ulaya na kufanya kazi kwa karibu na uongozi wa Ujerumani kwenye Baraza la Umoja huo wa Ulaya kusukuma ajenda zenye manufaa na maslahi kwa pande zote mbili.

No comments :

Post a Comment