Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Mhandisi Masanja Kadogosa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kurejesha huduma za usafiri wa Train kutoka Arusha-Dar es Salaam utakaoanza Oktoba 2 mwaka huu.
*Baada ya miaka 30 wananchi kuona huduma hiyo
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV.
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetangaza kuanza Safari za Train kwa
kuanzia Arusha -Dar es Salaam kuanzia Oktoba 2 mwaka huu.Akizungumza Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Mhandisi Masanja Kadogosa amesema kuanza kwa Safari hizo ni kusogeza huduma kwa wananchi na kuwarahisishia usafiri wa gharama nafuu.
Amesema kuwa usafiri ulikuwepo miaka 30 iliyopita lakini kutokana na mikakati ya serikali ya awamu ya Tano wameweza kurejesha huduma hiyo kwa wananchi.
Amesema kuwa katika Safari zitakazoanza zitakuwa na punguzo kwa asilimia 15 kwa kipindi cha mwezi mmoja.
Aidha amesema kuwa huduma ya train ya mizigo inaendelea na kusaidia katika usafirisha wa bidhaa mbalimbali katika Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro na wafanyabiashara wameishukuru kurudisha train hiyo.
Amesema huduma za usafiri zitakuwa ni endelevu ikiwa ni pamoja watalii kutumia huduma hiyo katika Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.
No comments :
Post a Comment