Wednesday, September 30, 2020

MKUU WA MKOA KILIMANJARO MGENI RASMI KONGAMANO LA WAJASILIAMALI,WANANCHI WAOMBWA KUJITOKEZA KWA WINGI

Na Jane Edward Arusha,Michuzi TV


Mwanamke Mtanzania mfanyabiashara aishiye Marekani(UK) ,Gladness Katega Amewataka wanawake na wanaume kujitokeza katika kongamano la

wajasiliamali linalotarajiwa kufanyika mnamo Oktoba 2 hadi 6 ili kujifunza na kujadili changamoto za kibiashara ili kuweza kupanua biashara zao na kumuinua mwanamke kiuchumi.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha,Katega alisema kongamano hilo litawasaidia  wanawake wa Tanzania katika kuinuka kiuchumi na kuweza kutanua biashara zao ikiwa lengo lao Ni kuona wanawake wakifanya biashara kwa pamoja kupitia ushirikiano wa umoja wao.


"Tunataka mwanamke kuinuka  kiuchumi kwa ndani na nje ya nchi  kwani wanawake wajasiriamali wakijitokeza wote na kufanikiwa  kupata elimu Kupitia mafunzo watajadiliana namna ya namna ya kukuza biashara kufikia  biashara nakufikia Mataifa mengine,"alisema Mkurugenzi huyo.


Katika kongamano hilo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira ambapo litadhaminiwa na wadau mbalimbali wakiwemo sunbright hotel,partner Africa Investment,na Kipina beauty saloon ikiwa Hadi Sasa wamejisajili wanawake kutoka nchi mbalimbali zaidi ya 90.


"Kila mwanamke na mwanaume audhurie ili kuwa na mitandao ya kibiashara nakujua namna ya upatikanaji wa masoko pamoja na kutatua changamoto ya namna ya kukuza na upatikanaji wa mitandao kwani ugonjwa wa covid umesitisha shughuli nyingi za kibiashara lakini Kupitia kongamano hilo litawasaidia kupata elimu zaidi,"alisema.


Kwa upande mwezeshaji wa mfunzo ya wanaume ya Kings master class kutoka nchini Kenya ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya RB,Robert Burale alisema wanaume wengi wanatunza  maumivu moyoni na kushindwa kuyasemea kwa watu kuhusu hali ya maisha kitu ambacho hupelekea wanaume kupoteza maisha kwa msongo mawazao.


"Kupitia mafunzo haya wanaume watazungumza maumivu yao yote na kuweza kupeana njia za kutatua ili kumfanya afurahie hali aliyonayo na kuweza kutatua matatizo na maumivu atunzayo moyoni  na kuweza kufanya shughuri zake zote,"alisema Burale.


Katika kongamano hilo watajifunza  pamoja nakutembelea maeneo ya hifadhi katika mbuga za wanyama na kubadilishana mawazo mbalimabali .



No comments :

Post a Comment