Mkuu
wa Mkoa wa Ausha akizindua rasmi Kampeni ya Elimu kwa Mlipakodi
iliyoanza rasmi tar.7sep2020 mkoa wa Arusha lengo likiwa ni kujenga
ukaribu kati ya TRA na wafanyabiashara.Afisa
msimamizi kodi mkuu James Ntalika kutoka kitengo cha Elimu kwa
mlipakodi TRA makao makuu Dar es Salaam,na Eugeni Mkubo kutoka TRA
Arusha wakitoa elimu kwa wafanyabiashara katika maeneo ya stendi ndogo
mkoani hapa. Robert
Tarimo mfanyabiashara wa duka na.360 ameishauri TRA mara baada ya
kupatiwa elimu ya mkipakodi kwamba kabla ya kuwakadiria kodi ni vyema
wakawatembelea ili waweze kuwakadiria kutokana na biashara zao Afisa
msimamizi kodi mkuu James Ntalika kutoka kitengo cha Elimu kwa
mlipakodi TRA makao makuu Dar es Salaam,akitoa elimu ya mlipakodi kwa
mfanyabiashara Alphonce Chaki katika eneo la stendi ndogo iliyopo Jijini
Arusha.Afisa
TRA kutoka makao makuu Jijini Dar es salaam Juliety Kidemi akiendelea
kutoa elimu ya mlipakodi kwa mfanyabiashara mwenye duka no 266 Maria
Hassan Matoto.Afisa
TRA kutoka makao makuu Jijini Dar es salaam Mercy Macha akiendelea
kutoa elimu ya mlipakodi kwa mfanyabiashara mwenye duka no 132 maeneo ya
stend ndogo Jijini Arusha .
TRA YAENDESHA ZOEZI LA ELIMU KWA MLIPAKODI ARUSHA
Na.Vero Ignatus.
Mamalaka
ya mapato imeendesha kampeni ya elimu kwa mlipa kodi kwa muda wa wiki
moja katika mkoa wa Ausha dhumuni kubwa likiwa ni kuhamasisha umma
katika uelewa wa masuala ya kodi ili waweze kutimiza wajibu wao kisheria
wa kulipa kodi
Akizindua
kampeni hiyo mkuu wa mkoa wa Arusha Idd Kimanta, amewasisitiza TRA
wahakikishe kwamba ,kampeni hiyo ya elimu kwa mlipakodi inafanyika
katika mkoa wote ,na wasikazanie mjini tu bali waende katika wilaya zote
6 ndani ya mkoa,sekta zote,zikiwemo za utalii ,kilimo ,ufugaji,na
wafanyabiashara wa aina zote na wananchi wote wanaopaswa kulipa kodi.
Alisema
kuwa kodi ya mapato inamanufaa makubwa kwa nchi ,ambapo miradi
mbalimbali imekuwa ikitekelezwa na serikali,amesema miradi mikubwa ya
kimkakati na ile ya kimaendeleo, inayosimamiwa na serikali kwa maelekezo
ya Rais Magufuli inatokana na kodi zinazolipwa
''Miradi
hiyo ni kama bwawa la umeme la Mwl.Nyerere,Treni ya mwendokasi,ununuzi
wa ndege kubwa za abiria ,ujenzi wa miundombinu ya barabara kama vile
fly overs za kuunganisha mikoa na ''Kimata
Kimanta
alisema ukusanyaji wa kodi unafanyika nchi nzima kupitia TRA,ambapo
mkoa wa Arusha ni miongoni mwa mikoa ambayo imekuwa ikifanya vizuri
katika makusanyo ya kodi, licha ya changamoto mbalimbali ,katika kipindi
cha mwaka uliopita 2019/20 walikusanya jumla ya shilingi Bil.420.83
ikiwa ni ongezeko la 12% ukilinganisha na kipindi kama hiki kwa mwaka wa
fedha uliopita.
Akizungumza
Afisa msimamizi kodi mkuu James Ntalika kutoka kitengo cha Elimu kwa
mlipakodi TRA makao makuu Dar es Salaam,anasema lengo lao ni kuweka
ukaribu kati yao na wafanyabiashara ambapo zoezi hilo ni la nchi nzima.
Amesema
ipo mikoa ambayo wameshaenda tayari ,kwa Arusha wameanza zoezi hilo
7sept 2020 na litafanyika katika katika wilaya zote na vitongoji vyake,
na watachukua maoni kwa wafanyabiashara,kushughulikia matatizo ya wadau
wao na kuwa daraja,pia amewataka kuondokana na ile dhana kwamba TRA ni
inatisha au kufunga maduka na kukimbia.
Amesema
mambo ambayo wanatolea elimu ya mlipakodi ni pamoja na utunzaji wa
kumbukumbu,mauzo kwa siku ,manunuzi na matumizi,hiyo itamrahisishia
mlipakodi kupata kodi stahiki wakati anafanyiwa makadiriao, kuliko
kukisiwa kwani atajikuta analipa kiasi ambacho sicho chenyewe.
Amesema
changamoto kubwa waliyokutananayo katika kuwatembelea wadau hao, ni
pamoja na kutokutungika TIN namba zao katika maeneo yao ya
biashara,wengine wanasema kuwa zipo nyumbani ama kwenye droo,hawatunzi
kumbukumbu.
Kwa
upande wake mfanyabiashara aliyepatiwa elimu ta mlipakodi na TRA Winnie
Frank ameiomba Mamlaka hiyo kuwaangalia kwani kodi ni kubwa kwa sasa
kulingana na kipato wanachokipata kwani biashara ni ngumu na wateja
hakuna
Amesema
wafanyabiashara wanakwepa na wanafunga maduka kwasababu kodi ni kubwa
sana kuliko kile wanachokipata,amewaomba TRA watoze kodi kulingana na
kile mfanyabiashara anachokipata itawarahisishia wao kulipa kodi.
Kwa
upande wake Robert Tarimo mfanyabiashara wa duka na.360 ameishauri TRA,
mara baada ya kupatiwa elimu ya mlipakodi, kwamba kabla ya kuwakadiria
kodi ni vyema wakawatembelea ,ili waweze kuwakadiria kulingana na
biashara wanazoziendesha.
''Sisi
wafanyabiashara tunavyokwenda pale,tunapoongea na wale maofisa pale
tunazungumza kulingana na biashara,mara nyingi hawatuamini kwamba
biashara ipo kama unavyowaeleza,kwahiyo naomba waje watutembelee kwenye
biashara zetu waangalie na yale makadirio''alisema Robert.
No comments :
Post a Comment