Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga
Bw. Albert Msovela akiongoza ujumbe wa Mkoa wa Shinyanga kutoa maoni kwa
wataalam wa TPDC walofika ofisini kwake kutambulisha mradi wa utafiti
wa Mafuta katika Bonde la mto Manonga eneo la Kishapu Mkoani Shinyanga.
Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa
Shinyanga wakifuatilia kwa makini ujumbe wa wataalam wa TPDC waliofika
Mkoani Shinyanga kwa kalengo la kutambulisha mradi wa utafiti wa awali
kuhusu utafutaji wa mafuta katika Bonde la Mto Manonga Wilaya Kishapu
Shinyanga.
Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa
Shinyanga wakifuatilia kwa makini ujumbe wa wataalam wa TPDC waliofika
Mkoani Shinyanga kwa kalengo la kutambulisha mradi wa utafiti wa awali
kuhusu utafutaji wa mafuta katika Bonde la Mto Manonga Wilaya Kishapu
Shinyanga.
…………………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu Shinyanga.
Shirika la
Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeanza hatua ya awali ya
utekelezaji wa mradi wa utafutaji wa mafuta katika bonde la mto Manonga
baada ya utafiti wa awali kubaini
uwepo wa miamba yenye viashiria vya
mafuta katika bonde la mto huo.
Mradi huo
ujalikanao kama EYASI –WEMBELE unatatekelezwa katika Mikoa ambayo mto
huo unapitia ikiwemo bonde la Ziwa EYASI na bonde la mto Manonga
unaopatikana katika Mikoa ya Tabora, Shinyanga, Singida na Manyara.
Akitambulisha
Mradi huo kwa uongozi wa Mkoa wa Shinyanga jana Mtaalam Mshauri wa Mradi
huo Dkt. Allan Mzengi kutoka TPDC alisema Mradi huo unaanza na hatua ya
awali ya kuangalia athari za kimazingira katika Wilaya Kishapu Mkoani
Shinyanga hatua itakayoshirikisha wadau kuanzia ngazi ya Mkoa hadi Kata.
Dr. Mzengi
aliuambia uongozi wa Mkoa wa Shinyanga kuwa pamoja na kuangazia suala la
kimazingira hatua ya pili ya mradi itakuwa ni ujenzi wa Mkuza katika
eneo ambao mradi huo utatekelezwa na baadae kuweka vilipuzi
vitakavyosaidia kubaini maeneo ya ujenzi wa visima vya majaribio ya
utafutaji mafuta katika eneo la mradi.
Aidha Mjilojia
Kutoka TPDC Bw. Gaston Canuty aliuambia uongozi wa Mkoa wa Shinyanga
kuwa tayari TBDC imeishachimba visima vifupi katika eneo la mradi
kubaini miamba yenye uwezekano wa kuifadhi mafuta na sasa mradi huo
unakusudia kwenda mbali zaidi kuangalia mafuta yako wapi chini ya Ardhi
baada ya kubaini miamba hiyo katika eneo la Kishapu.
Ili kufanikisha
zoezi hili Bw. Gaston aliongeza kuwa utafiti utatumia njia ya jiofizikia
ambapo watajenga mikuza ambayo itawekwa vilipuzi laini ambavyo
vitakapolipuliwa vitawawezesha kupata data chini ya ardhi
itakayowawezesha kutambua mahali penye uwezekano wa mafuta.
Bi. Loveness
Njogela ambaye pia ni Mjiolojia alisema utafiti wa Mafuta katika eneo
la Mradi ulianza kwa tumia ndege ya utafiti ambayo iliwawezesha kuona
maeneo yenye miamba yenye tabaka gumu na ile ya tabaka laini na kwa
kanuni za kijiolojioa maeneo yale ambayo yana mkandamizo mkubwa wa
miamba tabaka ndiyo yatakayofanyiwa jaribio la utafutaji mafuta.
Bi. Njogela
aliongeza kuwa pamoja na baadhi ya maeneo kuwa na miamba yenye
mgandamizo mkubwa inayotumika kama sampuli mafuta yana tabia kuama
katika eneo la miamba hiyo na kutafuta mtego mahali pengine ndio maana
wataweka vilipuzi laini vitakavyowezesha kutambua ni wapi kuna uwezekano
wa kuwa na mtego wenye mafuta.
Wakati huo Katibu
Tawala Mkoa wa Shinyanga Bw. Albert Msovela alihaidi kutoa ushirikiano
wa kutosha kwa wataalam hao kwa lengo la kufanikisha utafiti huo ambao
utafanyika katika kata za Mwamalasa, Gana na Mwamashele Wilayani Kishapu
Mkoa wa Shinyanga.
No comments :
Post a Comment