Kaimu
Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw.David Ndibalema
akikabidhi leseni na vyei kwa wazalishaji ambao bidhaa zao
zimethibitishwa ubora baada ya kukidhi matakwa ya Viwango kwa kipindi
cha kuanzia Mwezi Aprili hadi Juni mwaka huu.
Baadhi
ya wazalishaji ambao bidhaa zao zimethibitishwa ubora baada ya kukidhi
matakwa ya Viwango kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Aprili hadi Juni mwaka
huu.
**********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Shirika la Viwango Tanzania (TBS)
limetoa leseni na vyeti 167 kwa wazalishaji ambao bidhaa zao
zimethibitishwa ubora baada ya kukidhi matakwa ya Viwango kwa kipindi
cha kuanzia
Mwezi Aprili hadi Juni mwaka huu.
Akizungumza katika hafla hiyo
iliyofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo Jijini Dar es Salaam, Kaimu
Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw.David Ndibalema
amesema Vyeti na leseni hizo ni za bidhaa za vyakula,Vipodozi, Vifaa vya
Ujenzi,Vilainishi,Vitakasa Mikono,Vifaa vya Umeme, Vifaa vya Makenika,
magodolo, Vibebea pamoja na Vifungashio.
Aidha Bw.Ndibalema amewishukuru
Serikali kwa kuwahudumia wajasiriamali wadogo kupitia huduma za TBS juu
ya udhibiti ubora bila malipo ya gharama za ukaguzi na upimaji.
“Wajasiriamali hawa wataendelea
kuhudumiwa bure kwa kipindi cha miaka mitatu ya mwanzo.Hata baada ya
miaka mitatu kuisha,TBS itafanya tathimini ya uwezo wa wajasiriamali ili
kupima uwezo wao wa kulipa”. Amesema Bw.Ndibalema.
Hata hivyo Bw.Ndibalema amewahasa
wazalishaji hao waendelee kuzalisha bidhaa zinazokidhi matakwa ya
viwango kwa mustakabali wa afya na mazingira ya watumiaji kwa ujumla.
Nae amesema kama utahitaji
kusajili jengo lako la biashara utatembelea tovuti ya TBS ambao
kunamfumo wa kujisajili kwa njia ya mtandao kwa kuweka taarifa zako na
kuweza kupata akaunti ambayo itakusaidia kupata huduma ambazo hutolewa
na TBS katika mfumo wa mtandao.
Kwa upande wake mfanyabiashara wa
kampuni ya Woiso Original Products, wanaoshughulika na utengenezaji wa
viatu Bw.Joachim Komba amesema kampuni yao inajivunia kupata cheti
kutoka TBS kwani itatanua wigo kwa wateja wao kuwaamini na kutumia kitu
ama bidhaa yenye ubora wa hali ya juu.
Vilevile nae Afisa Masoko wa
kiwanda cha Yehehe Investment Limited Bw.Godlisen Mwanjala amesema mteja
anapohudumiwa na wafanyabiashara anatakiwa akiridhishe kwa kuoneshwa
leseni ili kujihakikishia bidhaa hiyo anayonunua imekidhi viwango na
inafaa kwa matumizi.
No comments :
Post a Comment