Mtafiti
kutoka Tari- Naliendele Programu ya Zao la Korosho, Kasiga Ngiha,
akitoa mafunzo ya jinsi ya kuandaa shamba, kulipima na upandaji wa zao
la korosho kwa Maafisa Ugani na Wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya
Kongwa katika shamba la Shule ya Sekondari ya Mnyakongo.
Mtafiti
kutoka Tari- Naliendele Programu ya Zao la Korosho, Kasiga Ngiha,
akitoa mafunzo ya jinsi ya upimaji wa shamba kabla ya kupanda korosho.
Afisa
Kilimo kutoka Kata ya Songambele, Asha Malekela wa Wilaya ya Kongwa
akipima shamba kwa kamba katika mafunzo hayo kwa vitendo.
Maafisa Ugani na Wakulima wakijifunza kwa vitendo namna ya upimaji wa shamba la korosho kabla ya kupanda.
Mkulima
Gasper Rupia kutoka Kijiji cha Ibwaga, akijifunza namna ya kupima
shamba wakati wa mafunzo kwa vitendo. Kulia ni Mkulima Raheli Esau
kutoka kijiji hicho.
Afisa
Kilimo, Said Kajagale kutoka Kata ya Ngomai akijifunza kunyoosha
mstari kwa kuelekeza kwa mkono katika mafunzo hayo ya vitendo.
Afisa Kilimo kutoka Kata ya Mkoka, Marcelin Chingilile (kushoto) na wenzake wakiwa kwenye mafunzo hayo
Afisa
Kilimo kutoka Wilaya ya Kongwa, Elias Chilemue (kushoto) na wenzake,
wakijifunza kutoka TARI namna ya kuweka alama wakati wa mafunzo kwa
vitendo ya upimaji wa shamba la korosho.
Afisa
Kilimo kutoka Wilaya ya Kongwa, Dominica Swai (kushoto) akijifunza
namna ya kuweka mambo wakati wa mafunzo kwa vitendo ya upimaji wa shamba
la korosho.
Mratibu
wa Kitaifa wa Zao la Korosho kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo TARI
Naliendele Mtwara, Dkt.Geradina Mzena (kulia), akielekeza namna ya
kunyosha mstari kwa kamba katika mafunzo hayo.
Mkulima Richard Sanyaji
kutoka Kata ya Songambele , akishiriki mafunzo kwa vitendo kwa kuchimba
mashimo katika shamba hilo la mfano la korosho la Shule ya Sekondari
Mnyakongo.
Mkulima Gasper Rupia kutoka Kijiji cha Ibwaga, akijifunza namna ya kuchanganya udongo na samadi kabla ya kupanda korosho.
Afisa Kilimo kutoka Kata ya Chitego, Michael Edward, akishiriki mafunzo kwa vitendo kwa kuchimba mashimo katika shamba la mfano la korosho la Shule ya Sekondari Mnyakongo.
Mtafiti wa Kilimo kutoka Tari Naliendele, Selemani Libaburu, akitoa mafunzo ya jinsi ya kupanda korosho katika shamba la mfano la korosho la Shule ya Sekondari Mnyakongo.
No comments :
Post a Comment