Saturday, September 5, 2020

TANESCO YAENDELEA KUTOA ELIMU KWA WACHIMBAJI WADOGO, VIWANDA NA MASHINE ZA KUSAGA NAFAKA


Mhandisi wa umeme kutoka TANESCO Hassan Kipende wa idara ya AMR mita akikagua miundo mbinu ya kiwanda Cha kuchakata mawe Cha even kilichoko chalinze mkoa wa Pwani.
Mashine ikichakata mawe katika kiwanda cha Even kilichoko Chalinze Mkoani Pwani.
 Kiwanda cha kusaga nafaka cha Energy Milling kilichoko Kibaha mkoani Pwani.

NA

NEEMA MBUJA, KIBAHA
Shirika
la umeme Tanzania TANESCO kupitia Idara ya masoko imeendelea na kampeni ya
kutoa Elimu kwa wamiliki wa viwanda,machimbo ya madini, na
mashine za kusaga
kwa mkoa wa Pwani ili kuwapatia Elimu juu ya matumizi Bora ya umeme sanjari na
kukagua miundo mbinu ya umeme pamoja na mota zinazotumiwa kwenye kuendesha
mashine
Miongoni
mwa Elimu wanayopatiwa Ni pamoja na namna ya kutumia vifaa ambavyo vinatumia
umeme kidogo, umuhimu wa kukagua mota zao Mara kwa Mara kwa ajili ya kuleta
ufanisi na Usalama wa miundo mbinu
Akizungumza
na wamiliki wa viwanda kwenye Wilaya za Chalinze, Mlandizi, na Kibaha, mhandisi
wa umeme kutoka idara ya AMR mita Hassan Kipende amesema kuwa kwa Sasa baadhi
ya  viwanda vinatambua umuhimu wa kufunga
power factor ingawa baadhi bado hawajatambua
Kuhusu
wachimbaji wadogo wa mawe eneo la Chalinze mhandisi Kipende ameshauri kuendelea
kuwapatia Elimu ya umuhimu wa kutumia umeme kwani wengi wao bado wanatumia
mafuta kuendesha mitambo ya kuchakata mawe Jambo ambalo Ni hasara kwao

No comments :

Post a Comment