Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George
H. Mkuchika akizungumza na Watumishi na wananchi wilayani Ngorongoro
kabla ya kuzindua jengo la Ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Ngorongoro
Septemba 04, 2020.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George H. Mkuchika akizindua jengo la
Ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Ngorongoro Septemba 04, 2020.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George H. Mkuchika akikata utepe kufungua
jengo la Ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Ngorongoro Septemba 04, 2020. Kulia
kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mhe. Rashid Taka na kushoto
kwake ni Mkurugenzi wa Uzuiaji Rushwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu
wa TAKUKURU,Bibi Sabina Seja.
Baadhi
ya Watumishi na wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro wakimsikiliza Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Kapt (Mst) Mhe. George H. Mkuchika alipokuwa akizungumza nao
kabla ya kuzindua jengo la Ofisi ya TAKUKURU Wilayani humo Septemba 04,
2020.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Kapt (Mst) Mhe. George H. Mkuchika akizungumza na Viongozi wa
Wilaya ya Ngorongoro ofisini kwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Rashid Taka
(wa kwanza kulia kwa Mhe. Waziri) alipoitembelea Ofisi hiyo kabla
ya kufungua jengo la Ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Ngorongoro Septemba 04,
2020.
Mkurugenzi
wa Uzuiaji Rushwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU,Bibi
Sabina Seja akitoa maelezo ya awali kuhusu jengo la Ofisi ya TAKUKURU
Wilaya ya Ngorongoro kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George H. Mkuchika kuzungumza na wananchi na kulizindua jengo hilo Septemba 04, 2020.
**************************************
Na. Mary Mwakapenda-Ngorongoro
Tarehe 04 Septemba, 2020
Watanzania wameaswa kushiriki
kikamilifu katika ujenzi wa taifa kwa kuzitumia vizuri Ofisi za Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) nchini ili kuwa chachu ya
maendeleo kwenye jamii wanayoishi, ikizingatiwa kuwa rushwa ikishamiri
katika taifa lolote lile huwa ni kikwazo kikubwa cha utekelezaji wa
miradi ya maendeleo.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapt (Mst)
Mhe. George H. Mkuchika wakati akiwasihi wananchi wa Wilaya ya
Ngorongoro kuitumia vizuri Ofisi ya TAKUKURU wilayani humo, aliyoizindua
rasmi Septemba 4, 2020.
Mhe. Mkuchika amesema, njia sahihi
ya kuleta maendeleo nchini ni ushiriki wa kila Mtanzania kuwafichua
wala rushwa na kutoshiriki vitendo vya rushwa, hususani katika Uchaguzi
Mkuu wa mwaka huu ambao taifa linategemea kupata viongozi bora wenye nia
ya dhati ya kuleta maendeleo.
Msishawishike kuomba rushwa wala
kupokea rushwa kwa lengo la kumchagua kiongozi wa chama chochote kile
cha siasa”, Mhe. Mkuchika amewaasa wananchi na kuongeza kuwa, uchaguzi
ukigubikwa na vitendo vya rushwa hautakuwa na tija kwa maendeleo ya
taifa.
Aidha, kuhusu azma ya Serikali
kuokoa fedha za umma, Mhe. Mkuchika ameipongeza TAKUKURU Mkoa wa Arusha
kwa kuokoa fedha kiasi cha shilingi Bilioni 2,490,396,226.00 katika
kipindi cha mwaka 2019/2020, fedha ambazo zitatumika kikamilifu kwenye
miradi ya maendeleo.
Kama mnavyofahamu mtazamo wa
mataifa kwa sasa ni kurejesha Serikalini mali zilizopatikana kwa njia ya
rushwa na ubadhirifu ili zitumike kwenye shughuli za maendeleo.” Mhe.
Mkuchika amefafanua.
Mhe. Mkuchika ameahidi kuwa,
Serikali itahakikisha TAKUKURU inaendelea kuimarika, hivyo amewataka
Watumishi wa TAKUKURU kuongeza juhudi katika kutekeleza jukumu lao la
kuzuia na kupambana na rushwa nchini.
Akitoa maelezo ya awali,
Mkurugenzi wa Uzuiaji Rushwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa
TAKUKURU, Bibi Sabina Seja amemshukuru Mhe. Rais kwa kuwajengea ofisi na
kuwapatia rasilimali za kutosha, hivyo ameahidi kuwa TAKUKURU itafanya
kazi kwa bidii kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa nchini.
Ufunguzi wa jengo la Ofisi ya
TAKUKURU Ngorongoro ni ushahidi wa namna Serikali ilivyodhamiria
kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa kwa kuiwezesha TAKUKURU kuwa na
ofisi itakayorahisisha utendaji kazi wake.
No comments :
Post a Comment