MSAJILI wa Hazina, Athumani Mbuttuka akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya semina elekezi kwa Mameneja wa Mikoa wa Shirika la Posta nchini yaliyofanyika kwa siku tano, jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Dk. Haruni Kondo,akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya semina elekezi kwa Mameneja wa Mikoa wa Shirika la Posta nchini yaliyofanyika kwa siku tano, jijini Dodoma.
Postamasta Mkuu Hassan mwang’ombe,akizungumza kwenye hafla ya kufunga mafunzo ya semina elekezi kwa Mameneja wa Mikoa wa Shirika la Posta nchini yaliyofanyika kwa siku tano, jijini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) Kitolina Kippa,akizungumza kwenye hafla ya kufunga mafunzo ya semina elekezi kwa Mameneja wa Mikoa wa Shirika la Posta nchini yaliyofanyika kwa siku tano, jijini Dodoma.
Kaimu Meneja Mkazi POSTA Zanzibar Bw.Khamis Swedi,akitoa neno la shukrani kwa Mgeni rasmi Msajili wa Hazina Athumani Mbuttuka (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya semina elekezi kwa Mameneja wa Mikoa wa Shirika la Posta nchini yaliyofanyika kwa siku tano, jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya semina elekezi kwa Mameneja wa Mikoa wa Shirika la Posta nchini yaliyofanyika kwa siku tano, jijini Dodoma.
MSAJILI wa Hazina, Athumani Mbuttuka akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kufunga mafunzo ya semina elekezi kwa Mameneja wa Mikoa wa Shirika la Posta nchini yaliyofanyika kwa siku tano, jijini Dodoma.
………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
MSAJILI wa Hazina, Athumani Mbuttuka amelitaka Shirika la Posta Tanzania kuweka mikakati ya kutengeneza faida zaidi ili kuongeza gawio kwa serikali.
Aidha, ameitaka Bodi ya Shirika hilo kuweka vigezo maalum vya kupima utendaji kazi wa Mameneja wa Mikoa kwenye makusanyo ili watakaoshindwa kukidhi waondolewe.
Mbuttuka, ameyasema hayo leo alipokuwa akifunga mafunzo kwa viongozi wa shirika hilo nchini yaliyofanyika kwa siku tano, jijini Dodoma.
Amesema kila tawi la shirika hilo lihakikishe linapata faida na washindane kwa kadri faida inavyotengenezwa ili kuongeza gawio kwa serikali.
“Hili gawio la Sh.Milioni 350 kwa ukubwa wa shirika hili, haiwezekani, tunatarajia kwa muda mfupi ujao tuanze kuzungumzia Bilioni na tunajua inawezekana,”amesema.
Hata hivyo, amesema kuna kamati yake ya ufundi inatengeneza mikataba ambayo itakuwa na malengo ya kupima shirika hilo.
“Tunataka tukikupima tukupime kwa kitu sahihi, katika muda mfupi ujao mtapata na kusaini mikataba mipya ili kuhakikisha kwamba shirika la posta linafanya kwa ufanisi kulingana na vigezo vya kupima ufanisi,”amesema.
Mbuttuka amepongeza shirika hilo kwa kutengeneza faida chanya tofauti na ilivyokuwa awali.
“Kwa miaka mitatu mfululizo mmejitahidi kutoa gawio miaka miwili mmetoa Sh.Milioni 350 kila mwaka, ule mwaka mwingine mmetoa Sh.Milioni 250, mnajua haitoshi, hivyo muweke mikakati ya kuongeza,”amesema.
Aidha, Msajili huyo amesema vimewekwa vigezo vya gharama za uendeshaji ambapo zinatakiwa zisizidi asilimia 50 lakini bado Shirika linajiendesha kwa gharama ya asilimia 75.
Naye, Posta Masta Mkuu Shirika hilo, Hassan Mwang’ombe, amesema mafunzo hayo yameweka mwelekeo mmoja wa utendaji kazi ambao kuna viwango vya ufanisi vimewekwa ambapo kila Meneja wa Mkoa anatakiwa awe amezalisha asilimia 75 ya bajeti Shirika.
Amesema dhamira ya shirika hilo ni kwa kinara cha utoaji huduma na kuna mikakati mbalimbali ya kufikia azma hiyo ambayo itaongeza utoaji wa gawio kwa serikali.
No comments :
Post a Comment