Sunday, September 20, 2020

RC- NDIKILO AIPONGEZA LAKE GROUP KWA KUANZISHA MRADI WA KUTENGENEZA MITUNGI YA GESI KIBAHA

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kulia akipata maelekezo kutoka kwa mmoja wa wakurungezi wa kampuni ya lake group inayotengeneza mitungi ya kesi Frank Nyabundege kushoto wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili  ya kukagua shughuli mbali mbali pamoja na kusikiliza kero na changamoto zinazowaakbili wawekezaji.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kati kati akiwa amesimama na baadhi ya viongozi wa kampuni ya lake group iliyojihusisha na utengenezaji wa mitungi ya gesi wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kutembelea baadhi ya viwanda vilinavyojengwa katika Wilaya ya Kibaha.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandis Evarist Ndikilo akitembelea katika kiwanda hicho cha Lake group  kwa ajili ya kujionea kazi mbali mbali ambazo zinafanyika katika kiwanda hicho ikiwa ni moja ya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kujionae mambo mbali mbali ambayo yanafanyika katika kiwanda hicho.

Mwonekano wa picha ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akiwa na watendaji wa kampuni la ya Lake Group wakiwa wanaangalia baadhi ya mitambo ambayo inatumika kwa ajili ya kutengenezea mitungi ya gesi.

************************************

NA VICTOR MASANGU,KIBAHA

MKUU wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amesema Uwekezaji wa Kiwanda Cha kutengeneza mitungi ya gesi unaofanywa na kampuni ya Lake Group utaondoa changamoto ya

uharibifu wa mazingira ndani na nje ya mkoa wa Pwani.

Ndikilo aliyaeleza hayo mwishoni mwa wiki baada ya ziara ya siku moja ya kutembelea baadhi ya Viwanda katika Halmashauri ya mji wa Kibaha.

Alisema, Kiwanda hicho ambacho ni cha kwanza hapa nchini mitungi itakayokuwa inatengenezwa itawafikia wananchi kwa urahisi na kwa Bei nafuu ukilinganisha na inayoagizwa kutoka nje ya nchi.

” Ukataji miti uliokithiri unakwenda kumalizika, uharibifu wa mazingira kutokana na matumizi ya kuni na mkaa sasa unaisha baada ya Lake Group  kuanzisha Kiwanda hiki ambacho kwa hapa nchini ni chakwanza” alisema Ndikilo.

Akitoa taarifa ya Kiwanda hicho Mkurugenzi wa Lake Oil Frank Nyabundege alisema, Kiwanda hicho ni kati ya Viwanda vinavyomilikiwa na kampuni ya Lake Group kikiwemo cha  Kiwanda cha, nondo, mambomba ya maji na cha mitungi ya gesi.

Nyabundege  alisema Kiwanda cha Lake cylinder( linachotengeneza mitungi) nikiwanda pekee Afrika Mashariki kinachozalisha mitungi ya gesi, ambapo kitakapokamilika katika awamu zote kitakuwa na uwezo wa kuajiri wafanyakazi 250 na katika awamu ya kwanza tayari wafanyakazi 25 wamepata ajira rasmi na 90 ni ajira zisizorasmi.

Alisema,Kiwanda hichoi kina uwezo wa kutengeneza mitungi 50,000  kwa mwezi na 600,000 kwa mwaka na kwamba mitungi hiyo ni asilimia 30 ya mitungi inayoagizwa hapa nchini

Alibainisha kampuni hiyo ya Lake Group kupitia Viwanda vyake vitatu vyote vikianza kufanya kazi vitakuwa na uwezo wa kulipa kodi  zaidi ya Bilion 2.8.

Mkuu wa Mkoa huyo alitembelea pia Kiwanda cha kutengeneza dawa za binadamu Cha Kairuki ambacho kikikamilika pia kitapunguza gharama za kuagiza dawa nje ya nchi.

 

No comments :

Post a Comment