Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Philip Chitaunga akizungumza na Wadau wa
Utalii wanaotoa huduma za malazi kwa Wageni katika mikoa ya Arusha,
Manyara na Kilimanjaro kabla ya kuanza kutolewa kwa mafunzo ya usajili
wa Wageni kwenye mfumo wa MNRT PORTAL yanayofanyika kwa muda wa siku
mbili kuanzia leo mkoani Arusha.
Baadhi
ya Wadau wa Utalii kati ya 250 wanaotoa huduma za malazi kwa Wageni
walioshiki kutoka katika mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro
wakifuatilia mafunzo ya usajili Wageni kwenye mfumo wa MNRT PORTAL
yanayoendelea kufanyika kwa siku mbili kuanzia leo mkoani Arusha.
SERIKALI
kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imewatoa hofu Wamiliki wa Huduma
za Malazi wa mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara kuwa usajili wa
Wageni kwenye mfumo wa MNRT PORTAL utakaoanza kutumika nchini kote
Oktoba 1, 2020 umelenga kupata takwimu sahihi za Wageni zitakazosaidia
katika kuboresha sekta ya Utalii nchini na si vingunevyo.
Pia,
Imesema Usajili huo utalinda siri za Wageni na zitatumika kwa ajili
ya matumizi ya Serikali pekee na sio kwa maslahi binafsi.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Arusha na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii,
Philip Chitaunga alipokuwa akihitimisha mafunzo yaliyofanyika kwa muda
wa siku mbili ya usajili Wageni kwenye Mfumo wa MNRT PORTAL kwa
Watoa Huduma za Malazi zaidi ya 250 wa mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na
Manyara.
Amesema
Usajili wa Wageni katika Mfumo huo utahusisha Wageni wa ndani pamoja na
Wageni kutoka nje ya nchi ambapo lengo kuu ni kupata takwimu
zitakazosaidia kuboresha sera, mikakati na mbinu za kukuza utalii
nchini.
Amesema
Usajili huo mbali ya kusaidia kujua idadi ya Watalii wa ndani bali
utawasaidia hata Wamiliki wa malazi hayo kuweka rekodi ya Wageni
waliolala katika malazi yao kwa kipindi chote ambacho anafanya biashara
hiyo ya malazi.
Chitaunga
amesema katika sekta ya utalii mfumo huo umekuwa ukitumika sehemu
nyingi Duniani kama vile Uingereza, Marekani na Kanada na si kitu kipya
kilichoanzishwa hapa nchini.
Pia
amesema mfumo huo utasaidia kurahisisha kazi kwa Wamiliki wa malazi
ambapo badala ya kubeba karatasi na kwenda katika ofisi za Wizara ya
Maliasili na utalii kwa ajili ya kulipia leseni ataweza kutumia
kompyuta yake akiwa ofisini kwake kufanya usajili huo.
Mkurugenzi
huyo amesema mfumo huo utakaonza kutumiwa na Watoa Huduma za malazi
nchini kote mwezi Oktoba 1, 2020 utahusisha hoteli, loji, nyumba za
Wageni pamoja na mahema ya watalii.
Ametaja
vitambulisho vitakavyotumika katika usajili huo kuwa ni Kitambulisho
cha Taifa kwa wageni ambao ni Watanzania na Pasi ya kusafiria kwa Wageni
wa kutoka nchi za nje.
Katika
hatua nyingine, Chitaunga amesema kuanza kutumika kwa Mfumo huo ni
utekelezaji wa takwa la kisheria linalomtaka kila Mmiliki wa Malazi
kuanza kusajili Wageni kwenye mfumo wa MNRT PORTAL.
Mbali
na hiyo, Chitaunga amesema matumizi ya mfumo huo utaifanya sekta ya
Utalii kwenda katika uchumi wa bluu utakaoiweka Tanzania katika
mazigira bora ya kibiashara.
Naye
Anne Sosteness ambaye ni miongoni mwa Wamiliki wa Malazi katika mkoa wa
Arusha aliyeshiriki mafunzo hayo, Amesema mafunzo ni mazuri na ni
salama kwa mteja na mtoa huduma kwa ssbabu Mteja anatakiwa kuonesha
kitambulisho chaTaifa au pasi ya kusafiria ili aweze kusajiliwa.
Aidha, Amesema mfumo huo unapunguza matumizi ya karatasi ambayo ni rahisi kupotea na kuchanika.
No comments :
Post a Comment