Ofisi
ya Rais - TAMISEMI imepokea maoni kutoka kwa wadau mbalimbali juu ya
changamoto za upatikanaji wa mtandao zilizojitokeza mara baada ya mfumo
wa kupokea maombi ya ajira ya walimu kufunguliwa rasmi tarehe 07
Septemba, 2020.
Tunapenda
kuwataarifu wadau kuwa kwa sasa changamoto hizo zimetatuliwa na mfumo
wa maombi ya ajira ya walimu umeongezewa uwezo na unapatikana kwa
urahisi zaidi.
Ili
kufidia kipindi ambacho kulikuwa na changamoto ya upatikanaji wa
mtandao katika mfumo wa maombi ya ajira ya walimu, Ofisi ya Rais –
TAMISEMI inapenda kuutangazia umma kuwa imeongeza muda wa kupokea maombi
ya nafasi za ajira ya walimu wa Shule za Msingi na Shule za Sekondari
na mafundi sanifu wa maabara za Shule za Sekondari kutoka
tarehe 21 Septemba, 2020 hadi tarehe 30 Septemba, 2020.
Hivyo,
Ofisi ya Rais - TAMISEMI inawatangazia waombaji wenye sifa kuendelea
kutuma maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia kiunganishi cha
https://ift.tt/3iPsolz (Online Teacher Employment Application System -
OTEAS) hadi tarehe 30 Septemba, 2020.
Sifa na vigezo kwa waombaji vitakuwa sawa na tangazo lililotolewa tarehe 07 Septemba, 2020.
Imetolewa na:
KATIBU MKUU
Ofisi ya Rais - TAMISEMI
18 Septemba, 2020
No comments :
Post a Comment