Wednesday, September 30, 2020

RAIS DK.SHEIN AKABIDHIWA RIPOTI YA KAMATI YA MADAWATI ZANZIBAR


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Madawati Zanzibar, baada ya kukabidhiwa ripoti ya Kamati hiyo na (kulia kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee na (kushoto kwa Rais) Mwenyekiti wa Kamati ya Madawati Zanzibar na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora na Utumishi wa
Umma Mhe.Haroun Ali Suleiman,hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa
Ikulu Jijini Zanzibar.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora na Utumishi wa Umma  na Mwenyekiti wa Kamati ya Madawati Zanzibar. Mhe. Haruon Ali Suleiman akizungumza wakati wa kukabidhi ripoti ya ukusanyaji wa madawati Zanzibar,mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar na (kushoto) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe.

RAIS wa Zanzibar n a Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akikabidhiwa ripoti ya ukusanyaji wa Madawati Zanzibar na Mwenyekiti wa Kamati ya Madawati Zanzibar na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora na Utumishi wa Umma Mhe. Haroun Ali Suleiman, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.

WAJUMBE wa Kamati ya Madawati  Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.(hayupo pichani) wakati hafla hiyo ya kukabidhi ripoti ya Kamati kwa Rais leo 30-9-2020 katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

No comments :

Post a Comment