Thursday, September 10, 2020

RAFIKI SDO YAKABIDHI VIFAA VYA UMEME KWA AJILI YA WATOTO WALIOKUWA WANAFANYISHWA KAZI MGODINI



Kulia ni Mratibu wa Mradi wa Kupinga Ajira za watoto Mgodini Tangi Clement kutoka Shirika la Rafiki SDO akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Hoja Mahiba vifaa vya umeme kwa ajili ya vijana 8 ambao awali walikuwa wanafanya kazi katika mgodi wa Mwakitolyo kisha kuchukuliwa na shirika la Rafiki SDO na kuwasomesha fani ya umeme,vifaa hivyo watavitumia kujitafutia kipato. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Kulia ni Mratibu wa Mradi wa Kupinga Ajira za watoto Mgodini Tangi Clement kutoka Shirika la Rafiki SDO akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Hoja Mahiba vifaa vya umeme kwa ajili ya vijana 8 ambao awali walikuwa wanafanya kazi katika mgodi wa Mwakitolyo kisha kuchukuliwa na shirika la Rafiki SDO na kuwasomesha fani ya umeme,vifaa hivyo watavitumia kujitafutia kipato.
Muonekano vya vifaa vya umeme vikiwa vimetolewa nje ya maboksi na vingine vikiwa ndani ya maboksi.
Kulia ni Meneja Msaidizi wa Shirika la Rafiki SDO, Charles Ally akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Hoja Mahiba vifaa vya umeme kwa ajili ya vijana 8 ambao awali walikuwa wanafanya kazi katika mgodi wa Mwakitolyo kisha kuchukuliwa na shirika la Rafiki SDO na kuwasomesha fani ya umeme,vifaa hivyo watavitumia kujitafutia kipato.

Meneja Msaidizi wa Shirika la Rafiki SDO, Charles Ally (wa pili kulia) akizungumza wakati shirika la Rafiki SDO likimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Hoja Mahiba (wa kwanza kushoto)  vifaa vya Umeme vyenye thamani ya shilingi milioni 1.75 kwa vijana nane waliokuwa wanafanya kazi katika mgodi wa Mwakitolyo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na kuhatarisha maisha yao ili wavitumie kupata kipato halali siyo kuhatarisha maisha yao mgodini leo Septemba 10,2020. Wa kwanza kulia ni Mratibu wa Mradi wa Kupinga Ajira za watoto Mgodini Tangi Clement, wa pili kushoto ni mmoja wa vijana waliosomea fani ya umeme, Said Malobe. 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Hoja Mahiba (kushoto) akitoa rai kwa taasisi mashirika mengine kuendelea kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto zilizopo katika jamii ikiwa kulinda watoto.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Hoja Mahiba (wa pili kushoto) akizungumza wakati wa makabidhino ya vifaa vya umeme.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Hoja Mahiba (kushoto) akimkabidhi Grill Said Malobe ambaye ni mmoja wa vijana waliopatiwa mafunzo ya umeme na shirika la Rafiki SDO kupitia Chuo cha maendeleo ya wananchi Buhangija.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Shirika la Rafiki Social Development Organization (Rafiki SDO) limetoa msaada wa vifaa vya
Umeme vyenye thamani ya shilingi milioni 1.75 kwa vijana nane waliokuwa wanafanya kazi katika mgodi wa Mwakitolyo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na kuhatarisha maisha yao ili wavitumie kupata kipato halali siyo kuhatarisha maisha yao mgodini.
Akikabidhi vifaa hivyo leo Alhamis Septemba 10,2020 kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Hoja Mahiba, Meneja Msaidizi wa Shirika la Rafiki SDO, Charles Ally amesema vijana/watoto hao walikuwa wanafanya kazi mgodini kisha kusomeshwa fani ya umeme na shirika hilo na sasa wamewapatia vifaa vya umeme ili waanze rasmi kujitegemea.
“Hawa vijana ni miongoni mwa watoto 10 waliokuwa wanafanya kazi katika mgodi wa Mwakitolyo,ndipo Rafiki SDO kupitia mradi wetu wa Kupinga Ajira za Watoto Mgodini ikafanya taratibu za kuwaibua kwa kushirikiana na viongozi wa serikali,tukawaambia kuwa tunahitaji kuwasaidia,wakatuambia wanahitaji nini ndipo tukawa na makundi mawili likiwemo la wale waliohitaji kusomea fani ya umeme na ushonaji wa cherehani”,ameeleza Ally.
“Tulipata watoto 10 kati yao, wawili walichagua kwenda kusomea fani ya ushonaji na wanane fani ya umeme ambapo wote walihitimu mafunzo yao katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Buhangija mwaka 2018. Baada ya kuhitimu na kurudi nyumbani,tukaona kuwa hatuwezi kuwaacha hivi hivi wakiwa hawana kitu cha kuanzia hivyo tuangalie namna ya kuwasaidia”,alifafanua Ally.
Amesema wamekabidhi vifaa 33 vyenye thamani ya shilingi 1,757,500/= vya umeme kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ambapo ofisi yake itaangalia utaratibu wa kukabidhi vifaa hivyo kwa vijana hao wanane waliosomea fani ya umeme ili wakakae pamoja waanze kufanya kazi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Hoja Mahiba amelishukuru Shirika la Rafiki SDO kujitokeza kuwasaidia watoto waliokuwa mgodini kwa kuwapatia vifaa vitakavyowawezesha kujitegemea kiuchumi badala ya kujiingiza katika maisha hatarishi.
“Niwashukuru sana Rafiki SDO, tumekuwa tukifanya nanyi kazi hasa kwa makundi ya watu wanaohitaji msaada. Kweli tuna changamoto ya eneo la Mwakitolyo kwa vijana wa kike na wa kiume ambao pengine kwa sababu ya mazingira wameacha masomo yao wakaenda kujihusisha na masuala ya uchimbaji madini”,amesema Mahiba.
“Niwashukuru pia kwa ajili hawa vijana wanane ambao mmewafundisha masuala ya umeme. Nashukuru zaidi kwa sababu mmetuongezea nguvu,tumepata wataalamu ambao wamefundishwa fani ya umeme, hata TANESCO watatambua kuwa Mwakitolyo kuna vijana wamepewa mafunzo na Rafiki SDO na wamewezeshwa vifaa na wana ofisi hivyo wanaweza kuwatumia”,ameongeza Mahiba.
Mkurugenzi huyo amesema sasa vijana hao watafanya kazi zao vizuri kwa sababu sasa wana ofisi rasmi wataweza kupata kipato ambacho ni halali siyo kama kile walichokuwa wanatafuta mgodini na kuhatarisha maisha yao
“Sisi kama halmashauri tunashukuru Rafiki SDO kwa kuwawezesha hawa vijana kwani mmewatoa katika hatua moja ya maisha iliyokuwa hatarishi na mmewajengea uwezo wa kujitegemea”,amesema. 
“Nitoa rai kwa taasisi mashirika mengine tuendelee kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto zilizopo katika jamii ambapo uwemo wa mila na desturi zimekuwa zikichangia watoto kutoka majumbani na kujiingiza katika vitendo hatarishi hivyo tushirikiane kuwaokoa watoto kutoka mazingira hatarishi”,amesema.
Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi wa Kupinga Ajira za watoto Mgodini Tangi Clement kutoka Shirika la Rafiki SDO amesema shirika la Rafiki SDO linatekeleza mradi huo kwa lengo la kuwatoa watoto wanaotumikishwa mgodini na kuangalia namna ya kuwapatia mafunzo ambayo yatawasaidia katika maisha yao.
“Mradi wa Mradi wa Kupinga Ajira za watoto Mgodini unalenga kuwatoa watoto wanaofanya kazi mgodini kwani kazi hizo zina athari kwa afya zao ambapo huwa tunawapeleka katika vyuo vya ufundi/Maendeleo ya jamii ili kuwasaidia waweze kujitegemea na kujitafutia kipato”,amesema Clement.
Miongoni mwa vifaa vya umeme vilivyotolewa na Shirika la Rafiki SDO ni Avo Meter,6mm PVC cable,main switch 4w TR, 2.5 mm PVC cable, Buble led low,gloves,helment,drill,leder, earth wire 1.5 mm, master tester, glasses, C/breaker TR, 1.5 mm cable, earth rod pure copper, earth wire 2.5 mm, socket TR, Two gang TR, one gang TR,patex box, trucking laine gundi, trunking gundi, conduit  pine nyeupe, conduit pipe africable,sadolle clip plastic 22mm, sadole clip plastic 8,9,10 mm, round box, insuration tape,round cover, saddle clip metal, temp holder TR na earth wire 2.5

No comments :

Post a Comment