
………………………………………………………………………….
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof.
Mabula Mchembe azindua kitambulisho cha wakaguzi wa dawa, vifaa tiba na
vutendanishi katika hafla ya uzinduzi iliyoenda sambamba na mafunzo ya
wakaguzi hao.
Uzinduzi huo ambao umefanyika
katika ukumbi wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) wa Kanda ya Ziwa,
jijini Mwanza ulihudhuriwa na wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wizara ya
Afya kwa TMDA, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Menejimenti, Wakaguzi toka
TMDA na Halmashauri mbalimbali.
Prof. Mchembe amewataka wakaguzi
kuzingatia macdill yao ya kazi katika kutekeleza majukumu yao ya
kiudhibiti kwani bidhaa za dawa, vifaa tiba na vitendanishi ni bidhaa
zinazohitaji umakini mkubwa na zisiposimamiwa vizuri madhara yake ni
makubwa kwa jamii.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
TMDA, Bw. Adam Fimbo wakati akieleza maelezo juu ya uzinduzi huo alisema
kuwa uzinduzi huo unafanyika kufuatia maboresho makubwa yaliyofanyika
katika kuhakikisha kitambulisho hicho kinawekewa alama za kiusalama
ambazo zimeunganishwa na mfumo wa taarifa za wakaguzi wa Mamlaka ambapo
kadish hiyo itawezesha kubaini wakaguzi feki.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri
ya Wizara ya Afya kwa TMDA, Bw. Erick Shitindi, alimhakimishia KM (
Afya) kuwa Bodi itaendelea kusimamia ipasavyo utendaji wa TMDA kwa
mujibu wa taratibu ili kulinda Afya ya Jamii
No comments :
Post a Comment