…………………………………………………………………..
Zaidi ya Bilioni 3
zinakusanywa kila mwaka katika Pori la Akiba la Lukwati/Piti lililopo
Mkonia Songwe chini ya Usimamizi wa Mamlaka ya Wanyamapori
Tanzania(TAWA), ambapo ni miongoni mwa mapori ya akiba 23
yanayosimamiwa na mamlaka hiyo.
Hayo yamesemwa na
Meneja wa pori hilo Bw. Jembe Chifuno mbele ya Kaimu Kamishna wa
Uhifadhi Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania-TAWA Bw. Mabula
Misungwi akiwa kwenye ziara ya siku tatu ya kikazi katika kukagua mapori
yanayosimamiwa na TAWA.
Aidha Bwana Chifuno
memueleza kaimu Kamishna Mabula kuwa pori hilo lina vivutio vingi vya
utalii wakiwepo wanyamapori mbalimbali ambao ni kivutio kikubwa cha
wageni wengi kutoka nchi mbalimbali duniani kote kuja kujionea wanyama
hao.
Hata hivyo Shughuli
za uwindaji ndio sababu kubwa iliyosababisha Pori hili kuwa kinara wa
ukusanyaji wa mapato, ambapo mwaka 2018 pori liliingiza Jumla ya Dola za
kimarekani 550,000 sawa na Tshs billioni 1.2 na mwaka 2019 ,waliingiza
Dola 632,000 sawa na Tshs. billioni 1.4.
Nae Kamishna Mabula
Misungwi baada ya kuelezwa hayo alionesha kufurahishwa na kuridhishwa na
jitihada zinazofanywa na watumishi wa pori hilo katika kutunza, kulinda
na kuhifadhi rasilimali za Taifa walizopewa kuzisimamia
Awari Wakizungumza
mbele ya Kaimu Kamishna huyo watumishi wa pori hilo walishauri mambo
mbalimbali ikiwemo Kuanzishwa kwa utalii wa picha kwani yapo maeneo
mengi rafiki kwa aina hiyo ya Utalii.
Mengine ni kugawanywa
kwa Pori katika Kanda kurahisisha utekelezaji mzuri wa majukumu yao
kwani pori lina ukubwa wa Kilometa za mraba 6,113 ambazo ni kubwa Sana
kiutendaji,Waliomba waongezewe vitendea kazi kama vile magari ya
doria,mahema na doria za anga kwa kutumia ndege za TAWA na Kuongeza
idadi ya watumishi.
Akijibu changamoto za
watumishi hao Kaimu Kamishna Mabula aliwapongeza watumishi kwa juhudi
kubwa walizofanya kulisafisha pori kwa kuimarisha ulinzi na kuwataka
waongeze juhudi na kuahidi kushughulikia changamoto zaidi kadri
wawezavyo ili kuongeza morali ya watumishi na mapato
No comments :
Post a Comment