Tuesday, September 29, 2020

NEC YAVITAKA VYAMA VYA SIASA NA WAGOMBEA WAO KUZINGATIA MAADILI YA UCHAGUZI

Makamu Mwenyekiti wa TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Mbarouk  S.Mbarouk,akizungumza wakati wa kufungua Mkutano wa Wadau wa uchaguzi Mkoa wa Dodoma.

Makamu Mwenyekiti wa TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Mbarouk  S.Mbarouk,akitoa maada kwa washiriki wa Mkutano wa Wadau wa uchaguzi Mkoa wa Dodoma.

Msimamizi wa Idara ya habari na Elimu kwa Mpiga kura Givness Haswile,akitoa taarifa wakati wa  Mkutano wa Wadau wa uchaguzi Mkoa wa Dodoma.

Mwenyekiti wa CPCT Dodoma Mjini Mchungaji John Maliga,akichagia maada kwenye  Mkutano wa Wadau wa uchaguzi Mkoa wa Dodoma.

Chief Mkuu Hert Mazengo,akielezea jambo kwenye Mkutano wa Wadau wa uchaguzi Mkoa wa Dodoma.

Afisa Sheria Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi.Fausta Mahenge ,akifafanua jambo kwa washiriki wa Mkutano wa Wadau wa uchaguzi Mkoa wa Dodoma.

Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Wadau wa uchaguzi Mkoa wa Dodoma uliofanyika leo jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi wa Usimamizi wa Rasilimali Watu  wa Tume ya Taifa ya Taifa ya Uchaguzi Leonard Tumua,akitoa neno la shukrani kwa washiriki wa Mkutano wa Wadau wa uchaguzi Mkoa wa Dodoma.

Makamu Mwenyekiti wa TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Mbarouk  S.Mbarouk,akiwa katika picha za pamoja mara baada ya kumaliza Mkutano wa Wadau wa uchaguzi Mkoa wa Dodoma

………………………………………………………………………………………………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

Makamu Mwenyekiti wa TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Mbarouk 

S.Mbarouk,amevitaka Vyama vya siasa na wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Urais,Wabunge na Madiwani kuzingatia maadili ya uchaguzi katika kipindi cha kampeni zao ikiwemo kuepuka lugha za kashfa na maneno ya uchochezi ambayo yanatishia  amani ya nchi.

Jaji  Mbarouk ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati alipokuwa akifungua Mkutano wa Wadau wa uchaguzi Mkoa wa Dodoma.

Aidha kunapokuwa na malalamiko yoyote ya kimaadili basi hatua stahiki zichukuliwe ikwemo kuwasilisha malalamiko kwenye kamati za maadili ndani ya muda uliowekwa’’ Amesema.
Aidha amesema Tume inaendelea kusimamia na kuendesha uchaguzi kwa kutumia sheria za uchaguzi hivyo vyama vya siasa,wagombe na wananchi wanakumbushwa kuwa  katika kipindi hiki sheria nyingine za nchi hazijasimama  hivyo wanapaswa kujihadhari na vitendo ama matamshi ambayo kusababisha vurugu kwa kisingizio cha uchaguzi.
‘’Tume inawahakikishia wananchi kuwa imejipanga katika kusimamia uchaguzi wa mwaka huu kwa kufuata katiba sheria,kanuni na miongozo mbalimbali na inaimani kuwa kila mdau akitimiza wajibu wake kwa kufuata taratibu watanzania wataweza kupiga kura kwa amani siku ya uchaguzi’’Amesema
Katika hatua nyingine tume imewatoa hofu wapiga kura  wenye mahitaji maalumu kuwa maelekezo yametolewa kwa watendaji wa uchaguzi kutoa kipaumbele kwa watu wenye ulemavu,wajawazito,akina mama wanaonyonyesha waliokwenda na watoto vituoni,wazee na wagonjwa.
‘’Kwa wasio jua kusoma na kuandika wanaruhusiwa kwenda na watu wanaowaamini kwa ajili ya kuwasaidia kupiga kura ,aidha kwa watu wenye ulemavu wa kuona kila kituo cha kupiga kura kutakuwa na kifaa cha maandishi ya nukta nundu  Tictile ‘’Ballot Folder’’ hiyo ni kwa wale wanafahamu kutumia maandishi hayo na kwa wasioweza wataruhusiwa kwenda kituoni na mtu anayemwamini wakuweza kumsaidia’’ Amesema
Hatahivyo, Jaji Mbarouk amesema kwa wenye ulemavu wa viungo vituturi vitakavyotumika kupigia vinaruhusu kuwahudumia kwani kuna pande mbili tofauti ambapo upande mmoja kuna urefu wa kutosha na kikigeuzwa kinakuwa kifupi kumuwezesha mwenye ulemavu wa viungo kupiga kura.

Naye Msimamizi wa Idara ya habari na Elimu kwa Mpiga kura Givness Haswile alipokuwa akimuwakilisha Mkurugenzi wa Uchaguzi amesema kuwa daftari hivi sasa lina jumla ya wapiga kura ikiwa ni jumla ya wapiga kura  29,188,347 ambapo wapiga kura 29,059,507 wapo Tanzania Bara na 128,840 wapo Tanzania Zanzibar.

“Pia kuna jumla ya wapiga kura 566,352 walioandikishwa na ZEC ambao watashiriki kupiga kura ya kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,alisema haswile.

Amesema kuwa Uboreshaji wa daftari la wapiga kura Tume imekamilisha uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura mara mbili kama inavyoelekezwa katika kifungu cha15(5) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi,sura ya 343 na kifungu cha21(5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za mitaa,sura ya 292.

Hata hivyo amesema kuwa  baada ya zoezi la uboreshaji wa daftari kwa awamu zote mbili wapigakura ambao taarifa zao zimejirudia na wale waliokosa sifa waliondolewa.

” Uboreshaji wa daftari kati ya wapiga kura 29,188,347 walioandikishwa ni wanawake 14,691,743 ambao ni sawa na asilimia 50.33,wanaume ni 14,496,604 sawa na asilimia 49.67,vijana kati ya umri wa miaka 18-35 ni 15,650,988 ikiwa vijana wa kiume ni 7,804,845 na wakike ni 7,846,153,

“Kuna jumla ya watu wenye ulemavu 13,211 na kati yao ni 2,223 wana ulemavu wa macho,4,911 wana ulemavu wa mikono na 6,077 wana ulemavu wa aina nyingine” amesisitiza Haswile.

 

No comments :

Post a Comment