Akiongea na waandishi wa habari jijini
Dodoma Septemba 5,2020 katika ofisi za Mfuko huo Mkurugenzi Mkuu Benard
Konga amesema taarifa hizo zimeleta taharuki kwa wanachama wake
Amesema mfuko huo umejenga imani kubwa
kwa wateja wake tangu kuasisiwa kwake mwaka 2001 kwa sasa una dawa 543
ambazo zikinyambulishwa zinafanya idadi ya dawa 975 baada ya kuongeza
kitita cha mafao mwaka 2016
Amewatoa hofu wanachama wa NHIF hapa
nchini na kuwataka kuendelea kutumia huduma hiyo na kutoa rai kwa
wananchi kuepuka kutoa taarifa ambazo si sahihi.
Septemba 4 mwaka huu zilisambaa taarifa
katika mitandao ya kijamii kuwa mfuko wa taifa wa bima ya afya
nchini(NHIF)umezifuta dawa 138 kutoka orodha ya dawa zinazotolewa na
mfuko huo kwa wanachama wake.
No comments :
Post a Comment