
Nchi
15 kupitia Balozi zao hapa nchini zimeruhusiwa kuleta waangalizi wa
Kimataifa katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Octoba, 2020
baada ya Balozi hizo kuwasilisha maombi na kufuata taratibu.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba
John Kabudi ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokutana na
kufanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya Balozi Manfred Fanti na
kuongeza kuwa uchaguzi wa mwaka huu kwa mara ya kwanza umekuwa tofauti
na miaka iliyopita kwa kuwa unafanyika kwa kugharamiwa na fedha za ndani
badala ya wahisani jambo ambalo baadhi ya watu walianza kuhofia
kutokuwepo kwa waangalizi wa kimataifa katika uchaguzi.
"Huu
ni uchaguzi mkuu ambao kwa mara ya kwanza kwa asilimia 100
tunaugharamia sisi wenyewe kama Serikali ya Tanzania, utaratibu wa
uchaguzi chini ya sheria ya uchaguzi na chini ya utaratibu wa Kimataifa
huwa tunakuwa na waangalizi wa uchaguzi na mwaka huu nchi hizo 15
kupitia balozi zao zimepata kibali mara baada ya kufuata taratibu za
kuomba kuleta waangalizi wa uchaguzi mkuu," Amesema Prof. Kabudi
Mbali
na Balozi wa Umoja wa Ulaya pia Prof. Kabudi amekutana na kufanya
mazungumzo na Balozi wa Italia hapa nchini Balozi Roberto Mengoni na
baadae Balozi wa Poland Balozi Krzysztof Buzalski ambapo amewakabidhi
vitabu vya sheria ya uchaguzi na kanuni za uchaguzi na miongozo
mbalimbali inayohusu masuala ya uchaguzi ili kuwapa fursa ya kufahamu
namna uchaguzi unavyoendeshwa hapa nchini hasusani baada ya uwepo wa
malalamiko kutoka kwa baadhi ya vyama vya upinzani juu ya kuenguliwa kwa
wagombea wao.
Kwa
upande wake Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini Balozi Manfred Fanti
amesema Nchi za Umoja huo zimekuwa zikifuatilia kwa karibu mchakato wa
kampeni za uchaguzi mkuu zinavyoendelea hapa nchini ambapo mpaka sasa
wanaridhishwa na kampeni zinavyofanyika kwa uhuru na amani na sasa
wanajiandaa na zoezi la uangalizi wa uchaguzi huo.
Balozi
wa Italia hapa nchini Mhe. Roberto Mengoni amesema amevutiwa na namna
vyombo vya habari vimekuwa vikitoa nafasi kwa wagombea wote kwa uhuru na
bila ya ubaguzi na kupongeza namna Watanzania wanavyojitokeza kwa wingi
kusikiliza sera za wagombea mbali na tishio la corona na kwamba ana
imani kuwa Kiongozi atakayechaguliwa atakuwa ametokana na utashi wa
wananchi.
Mbali
na masuala ya uchaguzi mkuu, Waziri Kabudi na Mabalozi hao wamejadili
pia masuala ya kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia,maendeleo ya
kiuchumi,biashara na uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwemo
elimu,afya,maji na miundombinu.
No comments :
Post a Comment