Baadhi ya Wataalamu wa Udahili ktoka chuo Kiku cha Waislamu Morogoro
wakiendelea na shghuli za dahili katika Maonyesho ya Vyuo viku katika
Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa viwanja vya maonesho ya vyuo vikuu Mnazi mmoja jijini Dar es salaam
Monekano wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro
…………………………………………………………..
Na. Hamadi Hassan, Dar es Salaam
Uongozi wa Chuo Kikuu cha Waislamu
cha Morogoro (MUM) umesema utaendelea kumuenzi aliyekuwa Rais wa awamu
ya tatu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati Benjamini
William Mkapa kwa mchango mkubwa aliotoa kwa Chuo hicho ikiwemo kutoa
majengo yanayotumiwa na chuo hicho.
Hayo yamesemwa na Afisa udahili wa
chuo hicho Abdulrahman Mumbu wakati Akizungumza na waandishi wa habari
waliofika katika banda la chuo hicho lililopo kwenye viwanja vya
maonesho ya vyuo vikuu Mnazi mmoja jijini Dar es salaam katika maonesho
hayo mwaka huu.
Mumbu amesema chuo hicho
kitaendelea kukumbuka mchango mkubwa uliotolewa na Hayati Mkapa ambao
umechangia kwa kiasi kikubwa uwepo wa chuo hicho.
Afisa habari wa chuo hicho Ngaja
Mchele amesema Chuo hicho kimejipanga kupokea maombi ya moja kwa moja
bila malipo yoyote kwa wanafunzi watakaotembelea banda la chuo hicho na
wale watakaotuma maombi yao kupitia tovuti ya chuo ambayo ni
www.mum.ac.tz.
Kwa upande wa Wanafunzi
wanaotarajia kujiunga na masomo ya elimu ya juu katika vyuo vikuu na
vyuo vya kati wamesema Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro kimeendela
kuwa Chuo pekee kinachotoa Elimu bora kwa kuzingatia maadili ya
Kitanzania.
Wamebainisha hayo walipotembelea
banda la Chuo hicho kwa lengo la kupata ufahamu kuhusu Chuo hicho na
kozi zinazotolewa ambapo baada ya kuridhishwa wamefanikiwa kufanya
maombi kwa ajili ya kujiunga na chuo hicho.
Latifa Omar na Zuwena Hemedi ambao
ni miongoni mwa wanafunzi waliofanikiwa kukamilisha maombi ya kujiunga
na chuo hicho katika fani ya Ualimu wamesema licha ya kuwa wanapenda
kuwa walimu lakini wamechagua MUM kuwa sehemu pekee itakayolinda maadili
na kuwa mahili katika fani zao.
No comments :
Post a Comment