Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi
ya maadimisho ya Siku ya Wahandisi kwa mwaka huu, Profesa Mwinyiwiwa,
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maadhimisho
ya siku hizo yanayotarajiwa kufanyika tarehe 3 na 4 mwezi Septemba, 2020
jijini Dodoma.
Msajili wa Bodi
ya Usajili wa Wahandisi, Mhandisi Patrick Barozi, akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokuwa akizungumzia kuhusu
maadhimisho ya Siku ya Wahandisi yanayotarajiwa kufanyika tarehe 3 na 4
mwezi Septemba, 2020 jijini Dodoma.
………………………………………………………………
Na. Alex Sonna, Dodoma
Mwenyekiti wa
maandalizi ya mkutano wa 17 wa Jumuiya ya Waandisi nchini, Profesa
Bakari Mwinyiwima amesema kuwa wahandisi zaidi ya 3,000 watashiriki
moja kwa moja , zaidi ya
2,000 watashiriki kwa njia ya matandao mkutano
huo.
Prof.Mwinyiwima ameitoa leo jijini
Dodoma wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya mkutano huo
unaotarajiwa kuanza tarehe 3 na 4 mwezi Septemba, 2020 jijini Dodoma.
Aidha Prof.
Mwinyiwima amesema kuwa katika mkutano huo wahandisi 550 wanatarajia
kula kiapo cha utii ili kwernda kutekeleza weledi wao kwa ufasaha.
Prof. Mwinyiwima
ameeleza kuwa Mkutano huo Bodi ya usajili wa wahandisi imewaalika
viongozi wa ngazi za juu serikalini, mashirika ya umma na binafsi,
wageni kutokna nje, wahandisi, makandarasali, wasanifu na wabunifu
majenzi, wanafunzi wanaosoma uhadisi na wadau mbalimbali kushiriki
kikamilifu.
“Miongoni mwa
wageni wa kimataifa watakao shiriki katika mkutano huo ni kutoka mataifa
ya wageni wanaotarajia kushiriki ni kutoka Zimbabwe, Kenya, Nigeria,
Uganda, Rwanda, Misri, Malawi, Botswana na Kenya”,.
Hata hvyo
Prof.Mwinyiwima ameweka wazi kuwa mkutano huo utajadili mada kuu ya
mapinduzi ya nne ya viwanda katika kufikia Malengo endelevu ya dunia:
changamoto na fursa kwa wahandisi utakuwa na manada nyingine 10 ambazo
zitaelezea mchango wa tekinolojia kutela tija kwenye kazi ya kiuhandisi.
Pia amesema kuwa watatoa tuzo kwa
taasisi zilizotia fora kwenye maonesho ya teknolojia na ubunifu,
maonesho ya biashara, maonesho ya huduma za kitaaluma na maonesho ya
uchuuzi
Kwa upande wake
Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Patrick Barozi amesema kuwa
mpaka sasa wahandisi 29,019 wamesajiliwa na Bodi hiyo.
No comments :
Post a Comment