Wajumbe
wa Menejimenti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiwa
katika eneo la kituo cha kupoozea umeme kwenye Reli ya Kisasa (SGR)
utakaotumiwa na treli.(Eleuteri Mangi, WHUSM).
Kwa hatua ya
awali mradi una manufaa makubwa na umetoa ajira kwa Watanzania asilimia
51 na wageni asilimia 49 tofauti na hapo awali ambapo ilipangwa
wataalamu wa ndani wawe asilimia 20 na wataalamu wa nje ya nchi wawe
asilimia 80.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Kipande cha Morogoro
Mkakutupora Singida, Mhandisi Mteshi Tito kwa wajumbe wa Menejimenti ya
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakati wa siku ya pili ya
ziara yao ya kutembea mradi huo na kuongeza hatua hiyo ya uwiano huo wa
ajira imefikiwa baada ya Watanzania kuonesha uwezo mkubwa wa uelewa
kwenye masuala ya reli.
Aidha, mradi huo unaendelea kutoa ajira
kwa watanzania katika maeneo yao ambapo unapita ikizingatiwa ni mradi
mkubwa unaopitia mikoa mingi inapopita reli kuanzia Dar es salaam,
Pwani, Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Mwanza na Kigoma
ambapo unatarajiwa kufika
Mafundi
wakiendelea na kazi ya kukamilisha miundombinu ya kupozea umeme
utakaotumika katika mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) nchini.(Eleuteri
Mangi, WHUSM).
Mbali na hayo mradi pia unatarajiwa kutoa fursa
nyingi za kiuchumi ambapo utasaidia kusafirisha mizigo kwenda nchi
jirani zisizo na bandari ikiwemo Burundi, Rwanda, Jamhuri ya
Kidemokrasiaya Kongo na Uganda hatua itakayosaidia kuchochea kukua kwa
uchumi wa nchi.
Wajumbe
wa Menejimenti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
wakipata maelezo kabla ya kupanda treni ya majaribio inayotumia umeme
wakati wa ziara yao ya kutembelea mradi wa Reli ya Kisasa (SGR)
unaotekelezwa na Serikali nchini.(Eleuteri Mangi, WHUSM).
Akimwakilisha
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mhandisi Masanja
Kadogosa, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Jamila Mbaruku
amewapongeza wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo kuwa na moyo wa uzalendo wa kuthamini na kuchukua hatua
ya kujionea mradi unaotekelezwa na Serikali kwa fedha za ndani.
“Ninaamini
mtakuwa mabalozi na wajumbe wazuri kwa kuwatangazia Watanzania juu ya
mradi wetu huu wa reli ya SGR kwa kuwa ninyi ndiyo wizara yenye kuisemea
Serikali, mmeuthamini, mmethubutu na mmeweza kutembelea eneo lote
inapopita reli yetu kutoka kituo cha Ihumwa Dodoma hadi kituo kikuu eneo
la Posta jijini Dar es Salaam,”amesema Jamila.
Kwa upande wake
Mkurugenzi Msaidizi Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Zahara Nguga
amesema kuwa, kuna dhana potofu inayoenezwa na watu kuwa mradi huo
utawanufaisha wafanyakazi peke yao, la hasha, mradi huo utawanufaisha
pia wafanyabiashara na wakulima kutoka maeneo mbalimbali inapopita reli
hiyo.
“Hata wakulima, mtu anaweze kuwekeza Kilosa akatoka Dar es
salaam saa 11 asubuhi na saa 1 yupo Kilosa akisimamia mifugo, mashamba
na mazao yake na jioni anarudi Dar es Salaam kuimarisha maisha yake ya
ndoa. Huu ni mradi unawanufaisha watanzania wote,”amesisitiza Mkurugenzi
Msaidizi huyo.
Wakitoa neno la shukrani kwa niaba ya Wajumbe wa
Menejimenti ya wizara hiyo, Mkuu wa Idara ya Sera na Mipango, Petro
Lyatuu pamoja na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni, Leah
Kihimbi wamesema kuwa waliazimia kutembelea mradi huo kwa kuzingatia
wizara yao ndiyo yenye dhamana ya habari na mradi huo hauna budi
kutangazwa na vyombo vya habari ili kuwaelimisha na kuwapa uelewa
wananchi juu ya miradi inayotekelezwa na nchi yao.
Wajumbe
wa Menejimenti ya Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo wakipata
maelezo wakati wa ziara yao ya kutembelea Reli ya Kisasa (SGR) katika
eneo la kituo kikuu cha reli hiyo jijini Dar es salaam kinachojulikana
kama Tanzanite.(Eleuteri Mangi, WHUSM).
Lengo la ziara yao la
kuufahamu mradi huo limefikiwa kwa kuwa wamejionea malighafi
zinazotumika kuutekeleza zinatoka hapa nchini ikiwemo saruji na nondo
zinazozalishwa na viwanda vya Tanzania na baada ya kukamilika utakuwa na
manufaa mengi ikiwemo matumizi mazuri ya muda wa kusafiri ambapo muda
wa kusafiri kutoka Dodoma hadi Dar es salaam utakuwa ni saa tatu na
Morogoro hadi Dar es Salaam itakuwa ni dakika 90 sawa na saa 1:30.
Aidha,
wameongeza kuwa wamepanda treni inayotumia umeme inayotumiwa na
wahandisi kutekeleza majukumu yao na kusema ukiwa ndani ya treni hiyo
unaweza kuendelea kufanya kazi za ofisini bila kuwa na mtikisiko wowote
na kuongeza kuwa mradi umekuja umejali maisha ya watu kwa maana
watautumia na Shirika la Reli limejali vitu vya asili vya kuitamaduni
ikiwemo mito na miti ambayo wameitunza vizuri.
No comments :
Post a Comment