
*************************************
NA FARIDA SAIDY,MOROGORO
Katika kuhakikisha wanawake, watoto na watu wemyeulemavu,
wanapata haki zao za msingi za kisheria kituo cha Sheria na Haki za
Binaadamu kimeendelea kutoa elimu kwa wadau wanaoshughurikia maswala ya makundi hayo,kwa lengo la kuweka misingi bora kati ya serikali na wananchi.
Akizungumza katika Warsha iliyowakutanisha wadau mbalimbali wa
wanaoshughurikia maswala ya wanawake,watoto na watu wenyeulemevu Mkoani
Morogoro, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Sheria na haki za Binaadamu
BI Anna Henga , Amesema kuwa Moja ya Lengo ya Kituo Hicho Ni Kutatua
changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni pamoja na kuhakikisha
masuala ya Usawa wa Kijinsia yanazingatiwa katika jamii.
Aidha Bi Henga amesema semina hiyo inalengo la kujadili namna
yakukabiliana na changamoto zinazowakumba wanawake,watoto na watu wenye
ulemavu hususani waishio vijijini kwani wengi wao wamekuwa wakishindwa
kutambua haki zao, wakati wakikutana na vitendo cha unyanyasaji.
Naye Mrakibu Mwandamizi kutoka Jeshi la Magereza SSP Amina
Kavirondo amesema kuwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali hasa kituo
cha Sheria na Haki za Binadamu imesaidia baadhi ya mamlaka kufanya kazi
kwa kufuata misingi ya Kazi hususani kutumia Sheria ipasavyo za kutetea
na kulinda haki za watoto na wanawake.
Kwa Upande wake Hakimu Mkazi
Mwandamizi kutoka Mahakama kuu Bi Rhoda Ngimilanga ameeleza kuwa katika
Mahakama zote nchini kesi za watoto zinapewa kipaumbele katika kufanya
Utekelezaji ulio thabiti kwa lengo la kupatikana kwa haki kwa muda
muhafaka.
Licha ya hayo imeelezwa kuwa Mwaka 2019 kituo kimeweza kufanya
Utafiti na kubaini haki za wanawake, Watoto na watu Wenye Uelemavu bado
zinavunjwa kwa kiwango Kikubwa ikiwemo Ulinzi wao Dhidi ya Ukatili ,
kingono, na hata kupelekea mauaji.
Warsha hiyo imehudhuriwa na wadau mbalimbli wanaoshughurikia
maswala ya wanawake,watoto na watu wenyeulemevu,wakiwemo Jeshi la
Polisi,Mahakama pamoja na Jeshi la Magereza.
No comments :
Post a Comment