Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha(IIA) Profesa Eliamani Sedoyeka akizungumza na waandishi wa habari.
Meneja
wa Tawi la Dar es Salaam wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IIA) Sekunda Titus
akizungumza wakati wa kumkaribisha mkuu wa Chuo hicho jijini Dar es
Salaam.
Mkuu
wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IIA) Profesa Eliamani Sedoyeka akizungumza
na waandishi wa habari kuhusiana na Chuo hicho kilivyojipanga katika
utoaji wa elimu bora yenye utaalam.
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
CHUO
cha Uhasibu Arusha (IIA) kimesema kuwa kimeongeza kozi 17 kutokana na
mahitaji kuongeza katika utoaji wa huduma utaalam kwa wananchi pamoja
kupanua uwigo wa soko la ajira
Akizungumza
Jijini Dar es Salaam Mkuu wa Chuo hicho Profesa Eliamani Sedoyeka
amesema kuwa kwa Tawi la Dar es Salaam wamehama jengo katika barabara ya
Pugu na Kuhamia katika Jengo la TTCL Kijitonyama ikiwa ni kusogeza
huduma kwa wanafunzi kwa urahisi wa kufikika.
Amesema
katika kozi zilizoongezeka ni pamoja ni lugha kwa Kichana kutokana na
kuwepo kwa wachina wengi wanaofanya miradi mbalimbali pamoja na watalii
ili waweze kuwasiliana nao.
Amesema
kati ya kozi ni pamoja ni kozi ya ujasiriamali kwani wengi wanafanya
biashara lakini hawana utaalam hivyo kozi itawajenga kuinuka kiuchumi
kwa kupangilia biashara zao.
Profesa
Sedoyeka amesema kuwa wanakozi za shahada ya pili ambazo shahada ya
Bima, Bank ambazo zitakafanya wawe wana utaalam zaidi katika utoaji wa
huduma kwa jamii.
Aidha
amesema pamoja na kuanzisha hizo kozi wameangalia upande wa waandishi
na kuweka kozi ya Multimedia ambapo katika eneo la mitandao ya kijamii
wataweza kumudu zaidi kuliko ilivyo sasa.
Profesa
Sedoyeka amesema Chuo licha ya kutoa elimu pia wanawajenga wanachuo
kimaadili ili elimu wanayaoipata iweze kuleta matokeo chanya katika
taifa.
Hata
hivyo Profesa Sedoyeka aliongeza kuwa kozi zote zilizoongezeka ni
kutokana na mahitaji ya soko huku kozi zingine zilizokuwepo zikiendelea
kuboreshwa.
Amesema
Chuo kimekuwa kinaongeza matawi yake katika kusogeza huduma kwa
wananchi pamoja na kuwa vpindi vinavyoanza mchana ili wafanyakazi waweze
kusoma kiurahisi.
Amesema
katika kipindi cha Ugonjwa wa Virusi vya IIA ilifunga Chuo lakini
walikuwa wanaendelea na vipndi kama kawaida kutokana mifumo ya mitandao
hadi wanachuo wakashauri kuendea kusoma kwa mtandao.
No comments :
Post a Comment