Elimu ya Mpiga Kura ni kwa ajili ya kuwaelimisha wananchi juu ya mambo ya msingi yatakayowawezesha kutekeleza kwa usahihi jukumu la kupiga kura Siku ya Uchaguzi Mkuu ambayo ni siku ya Jumatano, tarehe 28 Oktoba, 2020.
Na Christian Gaya, HakiPensheni Center.
Tume katika kutekeleza majukumua yake ya kikatiba, mwaka huu 2020 inaratibu na kusimamia uendeshaji wa Uchanguzi wa Rais, Wabunge katika Jamhuri ya Muungano na Uchaguzi wa Madiwani kwa Tanzania Bara. Kupitia kifungu 4C cha Sheria ya Taifa ya Uchanguzi, Tume imepewa mamlaka ya kutoa Elimu ya Mpiga Kura, kuratibu na kusimamia asasi na watu wanaotoa elimu hiyo.
Katika kutimiza matakwa ya kifungu hicho, Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura kupitia njia mbalimbali kama ya mtandao wa HakiPensheni kutoa Elimu ya Mpiga Kura kwa ajili ya kuwaelimisha wananchi juu ya mambo ya msingi yatakayowawezesha kutekeleza kwa usahihi jukumu la kupiga kura Siku ya Uchaguzi Mkuu ambayo ni siku ya Jumatano, tarehe 28 Oktoba, 2020.
Na lengo kuu la mkakati huu ni kutaka kuongeza kuaminika kwa Tume ya Taifa ya Uchanguzi katika kuandaa, na kuratibu na kusimamia uchaguzi, kwa kutoa habari na elimu ya Mpiga Kura kwa wakati na kwa usahihi katika michakato mbalimbali ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Malengo mahsusi ya kufanya hivyo ni kutaka kuongeza idadi ya wapiga kura watakaojitokeza siku ya uchaguzi, kupuguza idadi ya kura zinazoweza kuharibika, kuongeza ushiriki wa wadau katika michachato ya uchaguzi, na kupunguza hoja za malalamiko katika kipindi cha uchaguzi.
Kwa mfano elimu itolewayo kama vile ya uraia inamwezesha mwananchi kupata uelewa juu ya haki na wajibu wa raia kisiasa, kiuchumi na kijamii. Pia elimu itolewayo inamwezesha mwananchi kumpatia elimu pana ya kumjengea uwezo mwananchi kutambua mazingira yake na kuyamudu kwa kufanya maamuzi yanayomfaa, ambapo inaweza kuwezesha kuanza kujiuliza maswali kama vile nijiandikishe? au nigombee? Na kwa upande mwingine elimu ya uraia inaweza kumshawishi mtu kujiuliza maswali kama haya: kwa nini nishiriki kampeni? Na kwa kwa nini nipige kura?
Lengo la kutoa elimu ya mpiga kura ni kutaka kuwawezesha wananchi kupata uelewa wa sheria, kanuni, taratibu za uchaguzi, wajibu wao na umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi.
Elimu ya mpiga kura ni muhimu kwa mwananchi ili kuondoa fikra au hali ya kupuuza au kutofuatilia masuala ya uchaguzi. Hivyo basi elimu inamwezesha mpiga kura kuona umuhimu wa uchaguzi na kufuata mazingatio yake.
Pia lengo la kumpatia elimu mwananchi ni kutaka kuongeza ushiriki wa wapiga kura ya uchaguzi. Hivyo basi elimu kwa upande mwingine inawezesha wapiga kura kuthamini haki yao ya kuchagua viongozi na hivyo kuepuka kuipoteza.
Hivyo ifahamike wazi ya lengo la kutoa elimu ya mpiga kura kwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2020 ni kutaka kuhabarisha au kutoa habari za uchaguzi kwa wananchi, kwa mfano zinazohusu juu ya: Ratiba ya Uchaguzi Mkuu, michakato ya Uchaguzi, matokeo ya upigaji kura, mahali pa kupigia kura, haki na wajibu wa mpiga kura, n.k.
Pia ni kutaka kuwaelemisha au kutoa elimu kwa wananchi kuhusu sheria, kanuni, na taratibu za uchaguzi. Na kwa upande mwingine ni kutaka kuwahamasisha wananchi kushiriki kwenye michachato mbalimbali ya uchaguzi ikiwemo mikutano ya kampeni, upigaji wa kura n.k.
Na lengo lingine la mawasiliano ambalo ni muhimu ni kutaka kuwashirikisha wadau mbalimbali ikiwa ni kutaka kuimarisha mawasiliano na wadau mbalimbali wa Tume ili kuwezesha kila mdau kutekeleza wajibu wake katika kufanikisha uchaguzi.
No comments :
Post a Comment