Waziri
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani(mwenye shati la bluu) akisaini kitabu
cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye uzinduzi wa Usambazaji wa umeme
kwa kila kitongoji nchini uliofanyika katika Kitongoji cha Ufuruma,
Kijiji cha Ufuruma,Wilaya ya Uyui,Mkoani Tabora, Septemba
24,2020,(kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dkt.Philemon Sengati(kulia)
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati vijiji(REA)
Wakili Julius Kalolo.

Waziri
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa Kitongoji
cha Ufuruma, Kijiji cha Ufuruma,Wilaya ya Uyui,Mkoani Tabora,wakati
akiwa kwenye uzinduzi wa mradi wa Usambazaji umeme kwa kila kitongoji
nchini, uliofanyika Septemba 24,2020.

Moja
ya Mashine umba( Transifoma) ambayo bado haijakamilika ufungaji wake
ilizosimikwa na baadhi ya Kampuni za ukandarasi zinazotekeleza Mradi wa
Usambazaji wa Umeme katika Vijiji mbalimbali nchi.
*****************************************
Na Zuena Msuya na Hafsa Omari, Tabora
Waziri
wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amesema kuanzia sasa ni marufuku kwa
wakandarasi watakaotekeleza miradi Ya usambazaji wa umeme vijijini(
REA), kupewa kazi katika mikoa miwili na badala yake sasa watapewa kwa
kila wilaya bila kujali idadi ya vijiji vilivyopo.
Dkt.
Kalemani alisema hayo nyakati tofauti, mkoani Tabora alipokuwa
akizindua rasmi mradi wa usambazaji wa umeme katika kila Kitongoji
nchini uliofanyika katika wilaya za Uyui na Nzega mkoani humo, Septemba
24,2020 ambapo alisema kuwa mradi huo utavifikia vitongoji vyote nchini
bila kujali kuwa kimefikiwa na umeme au laa.
Alisema
kuwa lengo la kuwapatia wakandarasi hao kazi za wilaya ni kuhakikisha
kuwa miradi hiyo inakamilika kwa haraka ndani ya muda mfupi na kwa
wakati.
“Kuanzia
sasa Wakandarasi wote wanaotekeleza miradi ya REA nchini, watakuwa
wanapewa kazi za kutekeleza miradi hiyo kwa kila wilaya bila kujali
idadi ya vijiji vilivyopo,kwa maana kwamba mkandarasi anaweza pewa
wilaya moja yenye vijiji ishirini au sabini,jukumu lake ni kumaliza kwa
wakati, hii itaondoa changamoto ya kutomaliza miradi kwa wakati, au
wengine walikuwa wanaelekeza nguvu nyingi katika eneo A, na kuacha eneo
B, ama kufanya maeneo yote kwa kusuasua”, alisema Dkt. Kalemani.
Alieleza
kuwa utaratibu huo utawezesha ukamilishaji wa miradi ya namna hiyo kwa
wakati na kwamba mkandarasi yeyote atakayechelewesha mradi atachukuliwa
hatua za kimkataba, kisheria na za kiusimamizi kwakuwa maeneo ya
utekelezaji wa miradi imepunguzwa tofauti na awali.
Vilevile
alisema kuwa hakutakuwa na muda wa nyongeza kwa yeyote atayechelewesha
mradi na badala yake atakatwa asilimia 10% ya fedha zake kama adhabu na
mradi huo atapewa mtu mwingine.
“Hatua
hii itaondoa visingizio na sababu za baadhi ya wakandarasi wenye tabia
hiyo kwa lengo la kuchelewesha mradi, kwa sababu wengine walikuwa
wanasingizia ukubwa wa eneo, wengine miundombinu au vifaa havitoshi ana
kufika kwa wakati, sasa hii itamaliza sababu zote za kuchelewesha
miradi”, alisisitiza Dkt. Kalemani.
Katika
hatua nyingine, Dkt. Kalemani alilisisitiza Shirika la Umeme Tanzania(
TANESCO) kuwakatia umeme wateja wenye madeni sugu ili ikupata fedha za
kulijengea uwezo shirika hilo kutoa huduma bora na kufanya kazi kwa
ufanisi zaidi.
“Endapo
kuna Taasisi au Shirika la Umma linadaiwa ndani ya siku 14 msiwaoneee
aibu, nendeni makakate umeme, na wakiwapigia simu kuomba kurudishiwa
msikubali, na mimi nikipigiwa sitaruhusu waunganishwe hadi pale
watakapokuwa wamelipia”, alisema Dkt. Kalemani.
Aliwagiza
Mameneja wa Kanda, Mikoa Wilaya kutowaonea huruma wateja wa namana hiyo
kwa kuwa wanarudisha nyuma maendeleo ya shirika hilo na kusababisha
wananchi wengine kukosa huduma bora kwa wakati.

No comments :
Post a Comment