*************************************
Na Allawi Kaboyo Bukoba
Shirika lisilo la
kiserikali la World Vision Tanzania limetumia Zaidi ya shilingi Bilion
12 kwa
miaka 17 kuendesha miradi mbalimbali katika mradi wao mkuu
uliojulikana kama Kaerero AP halmashauri ya wilaya Bukoba mkoani Kagera
Kwa kuwanufaisha wananchi 28,671
Akiongea
katika hafla ya kuufunga mradi huo iliyofanyika Agost 26, mwaka huu na
kuhudhuliwa na Katibu tawala wa wilaya ya Bukoba Kadole Kilugala
aliyekuja kwaniaba ya mkuu wa wilaya hiyo pamoja na baadhi ya wananchi
wanufaika wa mradi Mkurugenzi wa miradi shirika la world vision
Tanzania John Masenza alisema,mradi wa kata Katerero umeweza kuhudumia
vijiji 10 na kata nne ambapo umenufaisha watu 39090 huku wanufaika wa
moja kwa moja wakiwa 28,671.
Masenza
alisema,wanufaika hapa wameweza kujifunza shughuli za kilimo, ufugaji
,ujasiriamali, uboreshaji wa afya maji na elimu na kugarimu shilingi
bilioni 12.7 kwa muda wa miaka 17 ya mradi huo.
Hata hivyo
alisema kuonekana kwa mafanikio hayo ni kwa ushirikiano wa Serikali na
shirika kwa ufadhili wa nchi ya Australia iliyokuwa ikitoa pesa ya
huduma hizo.
Katibu Tawala
wa wilaya Bukoba Kadole Kilugala alisema,ujuzi uliojengwa kwa
wananchi wa kata nne ndani ya wilaya hiyo,itasaidia kuwafaa kipindi
chote ambacho shirika halitakuwepo.
“Tambueni
mtu anaekupa ujuzi wa Jambo la kujitegemea Ni mzuri kuliko yule
anayekupa leo alafu kesho usimwone tena niwaambieni ujuzi huu utumieni
nyakati zote shirika linapokuwa halipo“alisema Kilugala
Vile vile
Kilugala alisema, mashirika yanayoleta ufadhili kwa jamii yanasaidia
kuongeza msukumo wa maendeleo kwani yanaweka mchango wake kwa Serikali
kusaidia jamii ambayo inauhitaji muhimu.,
BAADHI ya
Wananchi wa kata katerero wilaya ya Bukoba mkoani Kagera wameiomba
Serikali kuwapatia ufahamu wa jinsi ya kuendesha miradi ya maendeleo
kwa jamii inayoanzishwa na Serikali pamoja na wafadhiri mbalimbali ili
kuleta matokeo chanya yatokanayo na miradi hiyo.
Walisema
ufahamu huo utasaidia kuongeza sehemu ya kuelewa shughuli inayoletwa
kwa jamii Kama namna ya kusaidia katika uzalishaji mali ndani ya sekta
mbalimbali ambapo mradi huo ulikuwa ukihudumu kwenye kata za
Katerero,Bujugo, Kanyangereko na Kemondo.
Johanes Joel
mkazi wa kata Katerero alisema, miradi inayoletwa inawalenga wananchi
kuwabadilisha kwenye maisha na kupiga hatua ya maendeleo kwa kile
kinachokusudiwa.
“Bila kupewa
kwanza ufahamu inakuwa vigumu kuyafanya na kuonyesha mwitikio kwani
hatuna mwanga wa kuendesha wenyewe na kupata kitu chanya”alisema Joel
Jeneroza
Hamlungi mkazi wa kijiji Burinda kata Bujugo alisema,kuwa na wingi wa
miradi inategemewa wananchi kupewa elimu ya kufahamu jambo na kutoka
kwenye utegemezi wa ndugu na Serikali.
Aidha alisema
idadi kubwa mashirika yanatoa elimu wezeshi kwa jamii kabla ya
kuwapatia mradi na hukakikisha kundi linasimama lenyewe na kunufaika
Kama wanavyotegemea .
“Jamii
inamwitikio endapo itatambua kile kinacholetwa kinahitaji nini kwa Jami
na kufundisha na kufikia wengine wengine kutoa kwenye umasikini mi
napongeza mashirika “alisema Hamlungi.
Sharifa
Kakulwa mwenyekiti wa Kamati ya maendeleo ya Jamii kata Katerero
alisema kupitia shirika la world vision wananchi wameweza kuunda
vikundi zaidi ya 300 ambavyo vinanufaika na uchumi, kilimo,afya,
elimu, maji.
Aliongeza
kuwa,kundi la wanawake limeamka na kujiamini kuanzisha uzalishaji ambao
unawapatia kipato na kuendesha maisha yao tofauti na hapo awali.
No comments :
Post a Comment