Na Ismaily Luhamba Singida.
WAZIRI
wa Nishati Dkt. Medard Kalemani ametoa agizo kwa mkandarasi
anayetekeleza mradi wa kusambaza umeme vijijini REA awamu ya pili Mkoa
wa Singida pamoja na Shirika la umeme Tanzania TANESCO Mkoa huo
kuhakikisha wanamaliza mradi huo ifikapo Septemba 10 mwaka huu.
Ametoa
Agizo hilo jana wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi baada ya kutembelea
Kijiji cha Kisiriri kilichopo Wilayani Iramba Mkoni Singida ambapo
alikagua na kujionea kazi ya kusambaza umeme wa REA awamu ya pili ambapo
inafanyika kwa kusuasua.
Dkt
Kalemani aliitaka Kampuni ya JV MEMEC &DESCO ya Kitanzania
inayotekeleza Mradi huo kuwa ifikapo Septemba 10 mwaka huu wawe
wamekamilisha mradi huo.
“Nasema
hivi kuanzia leo hakuna mtu kurudi mjini hasa nyinyi wakandarasi,
mtabaki huku mpaka tarehe 10 nitakapo kuja mimi mwenyewe kwenye uzinduzi
na uwashwaji umeme katika Vijiji vyote 51 ili kumaliza huu mgogoro,
nawataka hawa wakandarasi Tanesco pamoja na Rea wawe wanakwenda kusaini
kila siku katika kituo cha Polisi kilichopo karibu na sehemu wanayo
fanyia kazi na mimi niwe napatiwa taarifa kila wiki”, alisema Kalemani.
Pia
Kalemani aliwataka Tanesco kuipima Kampuni ya JV EMEC & DESCO kwa
siku saba kama kweli wanaweza kumaliza kazi hiyo kwa muda aliyowapa, na
kama hawawezi kumaliza kwa wakati wavunje huo mkataba na kampuni hiyo.
Aidha ameipongeza kampuni ya CCCE ETERN CONSORTIUM LTD ya
Kichina ambayo inatekeleza mradi wa REA awamu ya tatu mzunguko wa
kwanza kwa kufanikiwa kusambaza umeme kwenye Vijiji 1680, ambapo
vimebaki vijiji 26 kwa Mkoa mzima ili kumaliza kazi ya kusambaza umeme.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa huo, Dkt Rehema Nchimbi amesema atahakikisha
anasimamia maelekezo hayo ili kabla ya muda uliopangwa na Waziri kuisha
mradi huo uwe umekamilika.
“Kupitia
kamati yangu ya ulinzi na usalama nitahakikisha mkandarasi anakwenda
kituo cha polisi kila siku na kusaini kama ulivyoagiza na ripoti hiyo
nitakutumia mimi mwenyewe”, alisema Dkt Nchimbi.
No comments :
Post a Comment