Friday, August 14, 2020

TCRA YAKIFUNGIA KIPINDI CHA JAHAZI CHA CLOUDS FM, YATOA ONYO RADIO FREE AFRICA,RADIO ONE, WASAFI

Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekifungia kipindi cha Jahazi Cha Clouds FM kwa kosa la kurusha maudhui yenye kuchochea kujichua sehemu za siri na ngono. Clouds FM imetakiwa kutokujaza muda huo kwa kipindi kingine chenye maudhui sawa na Jahazi.

Aidha Wasafi Media Online TV imetuhumiwa kurusha maudhui yanayochochea vitendo vya ngono kupitia kipindi cha Women Matters. Kosa la ngono kamati imetoa onyo na faini ya milioni 5 itakayolipwa TCRA.

No comments :

Post a Comment