Waziri
wa Madini Nchini Tanzania Dotto Biteko akizungumza katika mkutano mkuu
wa uchaguzi wa viongozi wawafanyabiashara wauzaji na wanunuzi wa madini
Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa Four Point (New Arusha Hotel)
Mwenyekiti
wa TAMIDA aliyemaliza muda wake akizungumza na wafanyabiashara ,wauzaji
na wanunuzi wa madini katika mkutano wa uchaguzi uliofanyika leo Jijini
Arusha .Picha na Vero Ignatus.
Waziri wa madini Dotto Boteko akisisitiza jambo kwa wafanyabiashara ,wauzaji na wanunuzi wa madini Tanzania
Baadhi ya washiriki wa mkutano wafanyabiashara ,wauzaji na wanunuzi wa madini Tanzania ,uliofanyika leo mkoani Arusha .
Baadhi ya washiriki wa mkutano wafanyabiashara ,wauzaji na wanunuzi wa madini Tanzania ,uliofanyika leo mkoani Arusha
Na.Vero Ignatus,Arusha
Waziri
wa madini Doto Biteko amewataka wafanyabiashara ,wauzaji na wanunuzi wa
madini Tanzania ,kufuata sheria na maelekezo mbalimbali ya serikali
,katika kufanya biashara zao, kutunza kumbukumbu,kuuza madini kwenye
masoko husika,sambamba na kujiepusha na vitendo vya utoroshaji madini.
Biteko
amesema kuwa Wizara ya madini imewabaini wafanyabiashara wakubwa nchini
12 wa madini ,ambao wanajihusisha na vitendo vya utoroshaji wa madini
nje ya nchi,amesema wamefanya kazi ya kuwafuatilia kwa miezi 3,ambapo
watoroshaji wamekuja na mbinu mpya ya kutumia magodoro,amesema serikali
haitalifumbia macho jambo hilo.
''Wewe
unaona kuna gari limekuja kununua magodoro Arusha,lakini wakati basi
lile linaondoka au lori,unawekwa na mzigo,ambapo ule mzigo ndiyo
unamaana zaidi kuliko hayo magodoro ,watanzania ni waaminifu wametupa
taarifa zote ''Alisema Biteko
Amesema
serikali ikimkamata mtu anatorosha madini haruhusiwi tena kufanya
biashara ya madini,hivyo amesema wanapomuona mtu anatorosha madini
wafahamu kuwa haibii serikali bali anawaibia watanzania kwa ujumla.
''Usalama
wako wewe ni kuiangalia sheria na kuizingatia ,usipofanya hivyo
utasumbuliwa hata na watu wa kawaida,utakuta mzee anasumbuliwa na katoto
first apointment ,lakini kama umezingatia sheria unamwambia wewe fanya
kazi yako,na bahati mbaya huko nje ya sekta watu wanaamini kuwa ninyi
mnapesa nyingi tena zisizo nakazi lakini hawajui humu ndani kuna watu
wanakunywa dawa za presha'' Alisema Biteko.
Amewataka
wafanyabiashara hao wamadini kuhama kwenye ule utaratibu wa kununua na
kuuziana, amewasisitiza kuondoka kwenye uchuuzi na kuingia kufanya
biashara ya madini,huku akiwataka kutunza kumbukumbu zao , kwani hakuna
hasara ya kutunza kumbukumbu, bali ipo faida kubwa kwani zitawasaidia
kwenda kwenye mabenki kwaajili ya kuombea mikopo ya kuendeshea biashara
zao
Aidha
Waziri Biteko amewataka TAMIDA kuchagua viongozi wenye weledi,waso
walalamishi,ambao watawaletea mrejesho baada ya kutoka kwenye Wizara,
anaweza kuwaambia ukweli hata kama wanamchukia,ambapo kupitia chama
hicho kiweze kuleta wafanya biashara kutoka mataifa mengine kwaajili ya
kununua madini.
Akizungumza
awali mwenyekiti aliyemaliza muda wake TAMIDA Sam Mollel alimpongeza
Mhe. Rais Magufuli kwa kuifikisha nchi kwenye uchumi wa kati miaka
mitano kabla ya 2025,udhibiti ukiwemo utoroshwaji na ulanguzi wa madini
na ujenzi wa ukuta wa Mererani ,pamoja na uanzishwaji wa masoko ya
serikali ya kuuzia na kununulia madini ,kwani kumeongeza mchango kwenye
pato la Taifa
Amesema
kuna changamoto ambazo hazijapatiwa ufumbuzi haswa ongezeko la thamani
VAT ya asilimia 18% kwenye (inter-dealer trade) na majengo
yanayopangishwa na wafanyabiashara wa madini,wakala wa meli Tanzania
TASAC,pamoja na mlolongo wa leseni katika biashara ya usonara .
Hivyo
ameuomba uongozi mpya utakaoingia madarakani baada ya uchaguzi utakuwa
na kazi kubwa kuanza na TASAC ili kuwashawishi wafanyabiashara wa madini
kufanya shughuli zao kwa uwazi kwa faida yao na Serikali.
Amesema
kuwa TASAC ikiondolewa na kuacha kujishughulisha na sekta ndogo ya
biashara ya madini itasaidia kuongeza kiwango cha usafirishaji wa madini
nje ya nchi ambapo fedha za kigeni zitaongezeka nchini na kuimarisha
uchumi wa nchi.
No comments :
Post a Comment