Mmoja
wa wanakikundi cha whatsapp cha wazawa wa Ludewa Sabinus Haule
(wakwanza kulia) akimkabidhi mahindi mkuu wa shule ya mahitaji maalum
Amos Mtitu ( wakwanza kushoto)
Wanakikundi cha wazawa wa Ludewa wakiongea na baadhi ya wanafunzi Katika shule ya mahitaji maalum
Magunia
70 ya mahindi na debe 11 za maharage waliyokabidhiwa uongozi wa shule
ya mahitaji maalum iliyopo Mundindi wilayani Ludewa kutoka kwa
wanakikundi cha Whatsapp cha wazawa wa Ludewa
Baadhi
ya madiwani waliopita kwenye kura za maoni ambao walijumuika na
wanakikundi hao, kutoka kushoto ni Edward Haule( Diwani kata ya Ibumi na
mwenyekiti wa Halmashauri aliyemaliza muda wake) , Wice Mgina (Diwani
wa kata ya Mundindi) pamoja na Vasco Mgimba (Diwani kata ya Ludende)
Baadhi
ya wanakikundi wakiwa kwenye picha ya pamoja na watendaji wa serikali
pamoja na walimu wa shule ya mahitaji maalum Mundindi
Baadhi
ya wanafunzi wanasoma shule ya mahitaji maalum Mundindi wakiwa na
walimu wao kwa ajili ya kupokea msaada wa mahindi na maharage kutoka
kwa wanakikundi cha Whatsapp cha wazawa wa Ludewa
Vasco
Mgimba ambaye ni Diwani aliyeshinda kura za maoni CCM kata ya Ludende (
wakwanza kulia) skifurahi na watoto wenye mahitaji maalum Katika shule
ya Mundindi
Mkuu
wa shule ya mahitaji maalum Mundindi, Amos Mtitu akisoma barua ya
shukrani kwa wanakikundi cha Whatsapp cha wazawa wa Ludewa baada ya
kutoa msaada wa gunia 70 za mahindi na debe 11 za maharage.
Na Shukrani Kawogo, Njombe.
Baadhi ya wazawa wa wilaya ya Ludewa mkoani Njombe ambao
wameunda kikundi cha Whatsapp chenye watu 194 wametoa msaada wa magunia 70 ya
mahindi pamoja na debe 11 za maharage katika shule ya mahitaji maalum iluyopo
wilayani humo katika kata ya Mundindi.
Wakikabidhi chakula hicho baadhi ya wanakikundi hao wamesema kuwa Katika mradi
wa shamba kikundi kilikodi shamba la ekari nane (8) ambazo kati ya hizo ekari
saba zilikuwa za mahindi na ekari moja ilikuwa ya maharage.
Waliongeza kuwa mchakato mzima umegharimu kiasi vha shilingi
ml. 4,238,000 ambapo mchanganuo wake ni kuanzia kukodi shamba kufyeka miti,kulima,
kupanda, kununua mbegu kupalilia na shughuli nyingine hadi kuvuna,kupiga na kufikisha
mazao shuleni.
Akipokea msaada huo mkuu wa shule hiyo Amos Mtitu amekishukuru
kikundi hicho kwa msaada huo na kuwaomba waendelee kuwa na moyo wa kusaidia
watu wenye uhitaji.
Kikundi hicho kina miaka sita tangu kuanzishwa kwake ambapo
mpaka sasa wameshatoa msaada katika sekta mbalimbali ikiwemo afya na elimu na
kinaongozwa na Yombayomba Yombayomba pamoja na Mwl. Benjamin Mtweve.
Hata hivyo kikundi hicho kinaendelea kuwakaribisha watu wote
wenye mapenzi mema na Ludewa kujiunga nao ili kuunga mkono harakati za kutoa
michango mbalimbali kwa jamii ili kukuza maendeleo.
No comments :
Post a Comment