Monday, August 31, 2020

WATENDAJI WIZARA YA MAJI WATAKIWA KUHAKIKISHA MAJI YANAPATIKANA KILA WAKATI KATIKA MAENEO YAO


KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga akizungumza na watendaji wakuu wa idara za Maji wakati  kikao kazi cha kutathimini utendaji kazi katika sekta ya Maji kilichofanyika leo  jijini Dodoma .
Sehemu ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga akizungumza na watendaji wakuu wa idara za Maji wakati  kikao kazi cha kutathimini utendaji kazi katika sekta ya Maji kilichofanyika leo  jijini Dodoma .
……………………………………………………………….
Na Alex Sonna,Dodoma
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga ametoa wito kwa watendaji wakuu wa idara za Maji kufanya kazi kwa ushirikiano ili kufikia lengo la kuwahudumia wananchi.
Aidha wito huo umetolewa leo kikao kazi cha kutathimini utendaji kazi katika sekta ya Maji Mhandisi Sanga amesema kuja baadi ya watendaji wanafanya kazi bila ushirikiano hali ambayo inaounguza tija katika kutoa huduma hiyo kwa wananchi.
“Maeneo mengi bado kuna umimi,naomba umimi huu tuumalize,tushirikiane katika utendaji wetu kwa ajili ya kufanya kazi yetu iwe bora zaidi katika kuwatumikia wananchi.” Amesema Mhandisi Santa
Mhandisi Santa amesisitiza kuwa watendaji hao kila mmoja kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana katika eneo lake .
Pia amewataka kusimamia miradi ya Maji inayongwa na kuhakikisha inajengwa kwa ubora na kwa thamani ya fedha inayotumuka katika mradi husika.
“Miradi msingi hivi sasa tunaitekeleza kwa fedha za” force account” sasa kama mradi unapaswa kukaa miaka 50 na iwe hivyo siyo mradi unajengwa kwa kutumiabfefha nyingi halafu baada ya muda kidogo unakuwa na nyufa,hii siyo sawa”ameongeza Mhandisi Santa 
Naye Katibu Mkuu Utumishi Dkt Francis Michael amesema watumishi wa Umma nchini hawana budi kuzingatia maadili ya utumishi Wa Umma na kuepuka mihemuko ya Kisiasa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 28 mwaka huu.
” Tunaelekea kwenye kipindi Cha Uchaguzi lazima tujue majukumu yetu nini sisi Kama watumishi wa umma hilo lazima kila mtumishi kulitambua bila kusahau uwadilifu,” amesisitiza Dkt Francis.
Aidha meongeza kuwa katika suala zima la siasa watumishi wa Umma wanahaki ya kidemokrasia kuchagua na kuchaguliwa au kuwa mwanacha wa Chama fulani Cha siasa nchini.
Kwa upande wake Naibu Mwanasheria Mkuu Serikalini  DAG Dkt.Evaristo Longopa…….kila mtu anahaki kikatiba kuchagua na kuchaguliwa na kutoa maoni yao.
Hata hivyo amesema katika ibara ya 20 kwenye katiba yetu inasema raia yoyote anahaki ya kushiriki na wenzake kwenye vikundi vya ushirika au vyama vya siasa.
“ ibara ya113 (a) inakataza majaji na mahakimu kujiunga na Chama chochote Cha siasa kwa sababu wenywe ndio watoa haki hivyo hawatakiwi kuwa  wanachama wa Chama Cha siasa”ameeleza .

No comments :

Post a Comment