Monday, August 31, 2020

DHULUMA ZA MIRATHI KWA WAJANE NI MIGOGORO INAYOHITAJI KUTAZAMWA KWA JICHO LA KIPEKE


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa LSF, Beng’i Issa,akizungumza wakati wa Mkutano wa shirika hilo unafanyika kwa siku tatu ulikutanisha mashirika 24 yasiyo ya kiserikali ambayo yanatoa huduma ya msaada wa kisheria Tanzania Bara na Zanzibar jijini Dodoma.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la kutoa msaada wa Kisheria nchini (LSF), Lulu Ng’wanakilala,akizungumza wakati wa Mkutano wa shirika hilo unafanyika kwa siku tatu ulikutanisha mashirika 24 yasiyo ya kiserikali ambayo yanatoa huduma ya msaada wa kisheria Tanzania Bara na Zanzibar jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wa Mkutano wa shirika la kutoa msaada wa Kisheria nchini (LSF),wakifatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kilimajaro Women Information Exchange Community Organization Bi.Elizabeth Minde akitoa mada kwenye Mkuu wa shirika la kutoa msaada wa Kisheria nchini (LSF) unafanyika  kwa siku tatu ulikutanisha mashirika 24 yasiyo ya kiserikali ambayo yanatoa huduma ya msaada wa kisheria Tanzania Bara na Zanzibar jijini Dodoma.
 
Mjumbe wa Bodi,Jenitha Kangura ,akizungumza  kwenye Mkuu wa shirika la kutoa msaada wa Kisheria nchini (LSF) unafanyika  kwa siku tatu ulikutanisha mashirika 24 yasiyo ya kiserikali ambayo yanatoa huduma ya msaada wa kisheria Tanzania Bara na Zanzibar jijini Dodoma.
………………………………………………………………………………..
Na. Alex Sonna, Dodoma
Migogoro ya ardhi na dhuluma za mirathi kwa wajane  ni migogoro inayohitaji msaada mkubwa wa kisheria nchini kwani imekuwa  ikiripotiwa kwa wingi kwa watoa huduma za msaada wa kisheria.
Inasemekana migogoro hiyo imekuwa ikitajwa kama tatizo kubwa  linalohitaji angalizi wa karibu wa  msaada wa kisheria ili kuweza kupungza migogoro hiyo.
Kauli hiyo ilitolewa leo Jijini Dodoma na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la kutoa msaada wa Kisheria nchini (LSF), Lulu Ng’wanakilala wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano mkuu wa shirika hilo.
Mkutano huo umeyakutanisha mashirika 24 yasiyo ya kiserikali ambayo yanatoa huduma ya msaada wa kisheria Tanzania Bara na Zanzibar.
Ng’wanakilala ameeleza eneo ambalo linahitaji “Sisi jukumu letu ni kutoa msaada wa kisheria bure nchi nzima na kwa miaka nane ambayo shirika limekuwa likifanya kazi zake tumeona eneo ambalo linahitaji msaada mkubwa wa kisheria ni kwenye ardhi kuna migogoro mingi huko.”
Ng’wabakilala amesema  wamekuwa wakipata  malalamiko mengi kutoka kwa wanawake ambao wanadhulumiwa mali na mirathi yao baada ya wenza wao kufariki dunia. 
Hata hivyo amesema kuwa  shirika hilo pamoja na kutoa msaada wa kisheria kwa watu wote lakini limejikita zaidi katika kutoa msaada kwa wanawake ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo waathirika wa kudai haki baada ya kudhulumiwa.
Kwa upande wake Meneja ufuatiliaji matokeo wa shirika hilo Said Chitung amesema  kutokana na uhitaji mkubwa uliopo wa watu wanaohitaji msaada wa kisheria waliamua kutoa mafunzo kwa watoa msaada wa kisheria 4,031.
Kwa kuongezea ameeleza kuwa  idadi hiyo ni ndogo kulinganisha na uhitaji uliopo kwani lengo lao ni kuwa na watoa msaada wa kisheria 6,000 nchi nzima ili kukidhi mahitaji yaliyopo.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa LSF, Beng’i Issa ameyataka mashirika hayo kuwafikia watu ambao wanataka kujishughulisha kwenye miradi ya kimkakati nchini na hawajui pa kuanzia.
Amesemakwa  hivi sasa serikali inatekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa, bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere lakini watu wengi hawajui jinsi ya kushiriki kwenye miradi hiyo kwa kuwa hawajui sheria inayowalinda

No comments :

Post a Comment