Saturday, August 15, 2020

Wanafunzi wa kitivo cha Habari Chuo kikuu cha Tumaini Wapigwa Msasa wa Sheria Mpya ya Habari

DAR ES SALAAM, Kufuatia kukithiri kwa ukiukwaji wa kanuni na misingi ya uandishi wa habari unaofanywa na waandishi wa habari kwasababu mbalimbali nchini ,Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania imelazimika kukutana na wanafunzi wa kitivo cha uandishi wa habari katika chuo kikuu cha Tumaini jijini Dar es salaam na kuwapa mafunzo kwa vitendo ya kuwajengea uwezo kuhusu kanuni,misingi na miiko ya taaluma hiyo.

Mkufunzi wa mafunzo hayo Adv Deogratus Bwire wakati akitoa elimu kwa wanafunzi wa chuo hicho kuhusu sheria za vyombo vya habari alisema lengo la kuendesha mafunzo hayo kwa wanafunzi waliopo vyuoni sasa ni kuwaongezea uelewa na uwezo wa utambuzi katika utekelezaji wa majukumu yao pindi watakapo hitimu na kuingia katika soko la ajira ambalo linahitaji umakini,ubunifu na weledi wa kiwango cha juu ili kukimbizana na mapinduzi ya sayansi na teknolojia.

“Wanafunzi wanapaswa kuzijua sheria zilizopo katika sekta ya habari pamoja na kukimbizana na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia ambayo imekuwa na mabadiliko ya mara kwa mara kwani kwa kufanya hivyo wanafunzi watakapohitimu na kuingia kazini watafanya kazi kwa kuzingatia maadili,kanuni na sheria za uandishi bila kukiuka katiba ya nchi”Alisema Adv Bwire.

Alisema waandishi wengi wa habari bado hawazijui sheria mpya za mitandao ya kijamii hivyo waandishi wanatakiwa kusoma kila mara ili kupukana na rungu la sheria kwa kosa la ukiukwaji wake huku pia akisema kinachowakuta waandishi ndicho kinachowatesa wananchi wanaofikishwa mahakamani baada ya kukutwa na kosa la kuvunja sheria mpya ya matumizi ya mitandao ya jamii.

“Hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la waandishi wa habari wanaochapisha maudhui ya habari mtandaoni kinyume cha sheria za mitandaoni ambazo zimetungwa hivi karibuni bungeni na kusainiwa na Rais wa Jamhuli ya Muungano wa Tanzania bila “alisema Adv Deogratus Bwire.
Muwezeshaji mwingine katika mafunzo hayo ni Joyce Shebe ambaye pia ni mhariri mkuu wa CMG ambaye aliwataka wanafunzi waliopo vyuoni kuwa makini na uandishi wa habari kwa

kuhakikisha wanaandika habari zenye mizania sawa ili kuondoa sintofahamu kwa walaji wa habari.

Aidha Shebe alisema katika sheria za mitandao tunapaswa kujiepusha sana kuonyesha sura za watoto au mtu aliyebakwa ama kufanyiwa ukatili wa aina yeyote ili kulinda utu na haki yao.

“Waandishi mkiwa kazini mnatakiwa kufanya kuzingatia maandili ya uandishi ili kuondoa migongano baina ya serikali na jamiii kulingana na aina ya habari iliofanyika” alisema Shebe.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo kutoka kitivo cha habari chuoni hapo wanasema mafunzo hayo ya siku tatu yamekuwa na tija sana kwao kwani yamewapa mwanga wa kwenda kukabiliana na changamoto zilizopo katika tasnia ya habari.

” Tunaendelea kujifunza misingi ya wanahabari ili kufanya kazi kwa weredi mkubwa wenye kuzingatia misingi na sheria za taaluma hii ambayo imekuwa na changamoto nyingi”

No comments :

Post a Comment