Saturday, August 15, 2020

UZINDUZI WA BENKI MPYA BAADA YA KUUNGANA KWA BENKI TATU (MWANGA,HAKIKA NA EFC BANK)

 


Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk.Bernad Kibesse (kushoto), Waziri Mkuu mstaafu Cleopa Msuya(katikati) wakifuatilia zoezi la uzinduzi wa benki ya Mwanga Hakika Microfinance Ltd.Benki hiyo ni muunganiko wa benki tatu (Mwanga Community bank, Hakika Microfinance Bank na EFC Tanzania Microfinance Bank).Kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa benki ya Mwanga Hakika Microfinance Ltd.

Naibu Gavana wa BoT, Dk.Bernard Kibesse akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi benki ya Mwanga Hakika Microfinance Bank iliyotokana na muunganiko wa benki tatu ikiwamo Mwanga community Bank,Hakika Microfinance Bank Pamoja na EFC Tanzania Microfinance Bank.Kulia kwake ni Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi, Eng.Ridhuan Mringo.

Naibu Gavana wa BoT, Dk Bernard Kibesse (Kulia), Naibu Mwekezaji, Raymond Tarimo pamoja na Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi Mhandishi Ridhuan Mringo wakifurahi baada ya kuzindua benki mpya iitwayo Mwanga Hakika Microfiance Bank baada ya muunganiko wa benki tatu tatu (Mwanga Community bank, Hakika Microfinance Bank na EFC Tanzania Microfinance Bank).Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Jagjit Singh.

4.Dk. Gabriel Ndunga, mteja wa kwanza kupata huduma kutoka benki mpya ya Mwanga Hakika Microfinance Bank iliyozinduliwa jana baada ya

kuungana kwa benki tatu ikiwamo Mwanga Community Bank,Hakika Microfinance Bank Pamoja na EFC Tanzania Microfinance Bank.

……………………………………………………………………..
 Hatua hiyo inatarajiwa kuongeza uimara wa benki katika utoaji wa huduma
pamoja na ubunifu.
Mwanga Community Bank Ltd, Hakika Microfinance bank Ltd na EFC Tanzania Microfinance zimefanikiwa kuungana na kuwa benki moja ijulikanayo kama ‘Mwanga Hakika Microfiance Bank Ltd’, hatua inayoashiria ukuaji wa sekta ya kibenki nchini.
Muunganiko huo umefanikiwa kufuatia uthibitisho kutoka benki ya Tanzania (BoT) pamoja na Tume ya ushindani (FCC) na kupelekea kuundwa kwa Benki moja yenye thamani ya 40.5 bilioni ya mali.Pia, benki hiyo inatarajia kuongeza nguvu ya ushindani katika soko nchini.
Muungano huo ulizinduliwa rasmi katika hafla iliyohudhuriwa na Naibu Gavana wa BoT, Dk.Bernard Kibesse na kushuhudiwa na wadau mbalimbali kutoka sekta ya fedha.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo, Eng. Ridhuan Mringo alisema muungano huo ni muhimu katika kuunda benki imara inayoweza kutoa huduma zenye viwango kwa wateja zenye kuzingatia unafuu na teknolojia za kisasa.
“Tunaamini kwamba huu ni muda wa Kuimarisha sekta ya kibenki na hii imejidhihirisha kwa baadhi ya benki ambazo ziliamua kuungana na kuunda benki moja imara.Sisi tumeamua kuungana ili kutengeneza benki kubwa na imara ambayo itasaidia kuongeza kasi ya ukuaji wa biashara yetu,” alisema Eng. Mringo.
Aliongeza kuwa kupitia benki hiyo wateja wataweza kupata huduma zilizoboreshwa zaidi na bidhaa zenye ubunifu katika mikopo na uhifadhi (savings) ambazo zitakuwa nafuu na za haraka.

“Kuanzia sasa mahitaji ya kila siku ya kibenki ya wateja wetu yataweza kutimizwa na benki hii mpya.Tunategemea kukua kwa makusanyo ya akaunti za wateja kwasababu benki hii itakuwa suluhisho la mahitaji mbalimbali ya kifedha,” alisema.
Kupitia muungano huo, benki mpya itaweza kuwa na mtandao mkubwa wa usambazaji huduma ikiwa na matawi saba (7) ambayo yataweza kuhudumia wateja 105,000 nchi nzima.
Naibu Gavana wa BoT, Dk.Bernard kibesse alipongeza hatua iliyochukuliwa na benki hizo na kwamba itasaidia katika uimarishaji wa sekta ya kibenki kwa kuhakikisha watu ambao hawajafikiwa na huduma wanapata nafasi hiyo.
Pia, alisema itasaidia katika kuchochea ukuaji wa uchumi kwani benki hiyo
na wigo mpana wa kutoa mikopo hasa kwa wajasiriamali wadogo na wa kati jambo litakalochangia kuleta ujumuishwaji wa uchumi.
“Sekta ya kibenki ni muhimu katika kuchangia maendeleo ya taifa kupitia ajira na kuchochea ukuaji wa biashara ndogo na za kati kupitia mikopo nafuu.Tunaamini
kwamba benki hii itachangia katika uimarishaji wa sekta hii na hatimaye kuongeza ujumuishwaji wa watu kiuchumi hapa nchini,”alisema Dk.Kibesse.

Takwimu:
Awali, Benki ya Mwanga ilikuwa na mali zenye thamani ya Sh21.6 bilioni huku Hakika benki ikiwa na 6.669 na EFC ikiwa na 12.253 bilioni na kufanya jumla ya benki hiyo kuwa na mali zenye thamani ya 40.5 billion. Kwa upande wa amana za wateja, Mwanga ilikuwa na 14.8 bilioni, Hakika 2.7 bilioni na EFC 5.96 bilioni.
Jumla ya mikopo ambayo imetolewa na benki hizo mpaka sasa ni 27.1 bilioni.

No comments :

Post a Comment