……………………………………………………………….
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
MKUU wa Mkoa wa Pwani
,Mhandisi Evarist Ndikilo amesema ,Mradi wa ujenzi wa Reli ya kisasa
(Standard Guage Railway-SGR) ni mradi wa kielelezo katika Taifa na
kwamba baadhi ya wananchi wa Mkoa huo ,wanaendelea kunufaika nao hasa
upande wa ajira .
Aidha ,kuhusu fidia
kwa ajili ya Taasisi na Wananchi waliopisha upanuzi wa Reli hiyo na
kutoa maeneo yao kwa ajili uchimbaji vifusi, Ndikilo amesema fedha
zimeshapatikana na wahusika wote wataanza kulipwa.
Akizungumzia
maendeleo ya ujenzi wa mradi huo eneo la Ruvu stesheni wilayani
Kibaha,alisema mradi huo mkubwa wa kimkakati umeshatoa ajira 300 za moja
kwa moja kwa wakazi wa Mkoa wa Pwani, huku makampuni makubwa Mkoani
hapo yamefaidika kwa kutoa huduma na bidhaa ambazo ni Nondo, Kokoto na
Chakula.
Aidha,Ndikilo alisema
Serikali kupitia mradi huo imejenga kituo cha kuhifadhia Mboga mboga
eneo la Ruvu stesheni( Freight station) hivyo uwepo wa kituo hiki
utaamsha ari ya kilimo cha mboga mboga katika bonde la Mto Ruvu na
kukuza biashara hiyo.
Hata hivyo Ndikilo
alieleza , Mkoa unaendelea kusimamia ulinzi na usalama wa mradi huo na
kwamba hakuna wizi mkubwa wa vifaa vya ujenzi.
“SGR inakwenda kuwa
mkombozi katika kurahisisha usafirishaji wa mizigo na watanzania hivyo
usafiri kuwa rahisi na uhakika kupitia njia ya reli ya kisasa”:; anasema
mkuu huyo wa mkoa .
Katika hatua
nyingine,maendeleo ya ujenzi unaendelea katika kipande cha kwanza na cha
pili katika awamu ya kwanza ya ujenzi Dar es salaam -Mwanza.
Katika kipande cha
kwanza Dar es salaam-Morogoro ujenzi umefikia asilimia 87 huku
Morogoro-Makutupora ujenzi wa reli umefikia asilimia 36.8.5.
No comments :
Post a Comment