Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia kutumia shilingi bilioni 331.7
kukamilisha uchaguzi mkuu utakofanyika Oktoba 28, 2020, ambapo fedha
hizo zitatolewa na serikali.
Mwenyekiti
wa NEC, Jaji Mstaafu, Semistocles Kaijage amesema fedha hizo zitatolewa
kupitia Mfuko Mkuu wa Hazina kwa kuzingatia kifungu cha 122 cha Sheria
ya Taifa ya Uchaguzi , hatua iliyopongezwa kwa serikali kugharamia
uchaguzi huo.
Jaji
Kaijage ameongeza kuwa jumla ya wapiga kura milioni 29.2
wamejiandikisha kupiga kura za madiwani, wawakilishi, wabunge na Rais.
Amesema
kutokana na idadi hiyo ya wapiga kura, kutakuwa na vituo 80,155 vya
kupigia kura na kila kituo kimoja kitahudumia wapiga kura wasiozidi 500.
No comments :
Post a Comment