Shirika
la afya duniani WHO limeonya jana kuwa janga la virusi vya corona
litadumu kwa muda mrefu na huenda likasababisha ''kulemewa kwa mikakati
ya kukabiliana nalo'' huku India na Ufilipino zikiripoti ongezeko la
maambukizi mapya.
Miezi
sita baada ya shirika hilo la WHO kutangaza janga hilo kuwa dharura ya
kimataifa, shirika la habari la AFP limeripoti kuwa virusi hivyo
vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 680,000 na maambukizi ya zaidi ya
watu milioni 17.5.
Kamati
ya dharura ya shirika hilo inayofanya tathmini mpya kuhusu janga hilo,
imesema janga hilo linatarajiwa kuwa la muda mrefu na kutaja umuhimu wa
kudumisha juhudi za kijamii, kitaifa, kikanda na kimataifa za
kukabiliana na virusi hivyo.
Katika
ujumbe kupitia mtandao wa twitter, shirika hilo la WHO limesema
linaendelea kukadiria kiwango cha hatari cha kimataifa cha COVID-19 kuwa
juu sana.
Credit: DW
No comments :
Post a Comment